Baada ya kutokea maafa Mfalme wa saudia ataka mageuzi hijja:
Mfalme Salman wa Saudi Arabia ametoa
agizo la kupitiwa upya kwa masuala ya hija baada ya watu zaidi mia saba
kufariki kutokana msongamano nje ya msikiti wa Macca.
Maafa hayo yalitokea mahujaji takriban milioni mbili walipokuwa wakishiriki moja ya kaida muhimu za mwisho katika ibada za hija.
Ndio mkasa mbaya zaidi kutokea wakati wa hija katika kipindi cha miaka 25.
Mahujaji husafiri hadi Mina wakati wa kuhiji kurusha mawe saba kwenye nguzo saba zijulikanazo kama Jamarat, ambazo huwakilisha shetani.
Nguzo hizo zimo katika eneo ambalo inaaminika Nabii Ibrahim alijaribiwa na shetani.
Watu walikuwa wakielekea eneo la kurushia mawe, na wengine wakitokea huko pale ghafla watu walipoanza kuanguka.
Kulikuwa na raia wa Nigeria, Niger, Chad na Senegal miongoni mwa mataifa mengine.
Idara ya ulinzi wa raia Saudi Arabia imesema mkanyagano huo ulitokea pale kulipotokea "ongezeko la ghafla" la watu waliokuwa wakielekea kwenye kwenye nguzo za kurushiwa mawe.
Waziri wa afya wa Saudi Arabia Khaled al-Falih amesema mkanyagano huo ulitokea kwa sababu mahujaji walikosa kufuata maagizo.
"Wengi wa wahamiaji huenda bila kufuata ratiba iliyowekwa," amesema.
Source: bbcswahili
0 Comments