Habari

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Advertise with us here

Diego Costa kukosa michezo mitatu

 
Diego Costa atakosa michezo mitatu baada ya chama cha soka cha England FA kuthibitisha kukutwa na makosa.
Costa alikana mashtaka yaliyokuwa yakimkabili kuhusiana na kumfanyia fujo mlinzi wa Arsenal Laurent Koscielny katika ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Arsenal.

Costa mwenye miaka 26 alionekana kuweka mikono yake juu ya uso wa Koscielny kabla ya kuanza kuzozana na Gabriel Paulista ambaye baadaye alitolewa nje kwa kadi nyekundu.
Mlinzi huyo wa Arsenal alitolewa nje na mwamuzi Mike Dean kwa kumfanyia vurugu mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Hispania.

Costa atakosa mchezo wa kombe la ligi dhidi ya Walsall siku ya jumatano sambamba na ile ya ligi kuu kati ya Newcastle na Southampton.

Baada ya kuthibitisha kuwa mwamuzi wa mchezo hakuona tukio la Costa na Koscielny, chama cha soka England kimesambaza kanda hizo za vidio kwa waamuzi wakongwe watatu wa zamani.

SOURCE: >> bbcswahili

Post a Comment

0 Comments

Youtube Channel Image
Hajiizo Subscribe To watch more
Subscribe