Headlines za leo kutoka Africa zinaandikwa na Bakary Yerima Bouba Alioum Mfalme kutoka Bafut, Kaskasini mwa Cameroon… Bafut ni moja ya sehemu ambazo ziko ndani ya Cameroon ziko chini ya utawala wa Kichifu.
Bakary Yerima Bouba Alioum ni
Mfalme wa kumi na moja wa Bafut aliyevaa majukumu ya Ufalme akiwa na
miaka 16 baada ya baba yake aliyekuwa Mfalme kufariki mwaka 1968,
amekuwa mfalme kwa zaidi ya miaka 47 sasahivi.
Mfalme Bakary
ana kitu kingine kikubwa ambacho kimefanya awe story leo, ana wake 100
na watoto zaidi ya 500… Kwenye moja ya Interview aliwahi kufanyiwa,
ameelezea sababu za yeye kuwa na wake wengi na watoto wote hao.
>>> “Wake
hawa wote hawakuwa wangu kuanza nao, nina wake watatu ambao nimewaoa..
hawa wengine wote nimewarithi baada ya baba yangu kufariki, wengine na
yeye aliwarithi baada ya babu yangu kufariki. Kimila, Mfalme akifariki
anayefuata kiuongozi anarithi wake zake wote.” >>> Mfalme Bakary.
>>> “Mila
zetu zinasema, ukiwa Mfalme wale wake wote wakubwa waliotangulia wana
jukumu la kumfundisha Mfalme mila na tamaduni hizi kwani Mfalme anakuwa
bado hajukua kuwa Mfalme” >>>
>>> “Malkia
kwenye himaya hii wanachukua nafasi kubwa sana, wanawake hawa
wanatakiwa kumjenga Mfalme wao ili aweze kuyamudu majukumu yake kama
Mfalme na pia kama mwanaume” >>>Mfalme Bakar.
Originated from >> millardayo
0 Comments