Habari

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Advertise with us here

UFAHAMU UGONJWA WA KUZIBA SIKIO NA MATIBABU YAKE.[CERUMEN IMPACTION]

katika hali ya kawaida sikio la binadamu hutengeneza utando unaovutika kama asali, utando huu huzuia uchafu kuingia ndani ya sikio, kulainisha sikio na kukamata wadudu wanaoingia ndani ya sikio..utando huu hutengenezwa kwa kiasi kidogo sana kwa siku ili kukizi mahitaji ya sikio kwa siku lakini katika hali isiyo ya kawaida utando huu unaweza kua mwingi sana na kuziba sikio na kumfanya mtu ashidwe kusikia vizuri.

                                                         
sio hivyo tu kuna sababu zingine mbalimbali ambazo zinaweza kuziba sikio la mtu na kulifanya lishindwe kusikia kama ifuatavyo..

  • matumizi ya vitu vya kuchokonoa sikio kama viberiti, kalama au pamba za masikioni.
  • kuziba kwa nywele ambazo hupatikana ndani ya sikio.
  • kuishi sehemu yenye vumbi sana
  • matatizo ya mirija ya masikio kitaalamu kama auditory canal
dalili za kuziba kwa sikio
  • maumivu makali sikioni
  • kushindwa kusikia
  • kuwashwa sikioni
  • kusikia kama sauti za kengere sikioni.
  • kizunguzungu
vipimo vipi hufanyika?
kwa kifaa maalumu kwa jina la otoscope daktari ataweza kuchunguza sikio na kuona kitu kilichoziba na kuweka mpango wa kukiondoa.
                                                     
 matibabu
dawa ya sodium carbonate au mafuta huanza kutumika na mgonjwa kwa kuweka matone mawili kwenye sikio husika kwa siku tatu mpaka tano ili kulainisha uchafu ulioganda sikioni kisha mgonjwa hutolewa uchafu huo kwa bomba maalumu hospitali.
angalizo; sikio kwa ndani ni laini sana, ukipata shida ya sikio usilete ujanja wowote wa kujitibu mwenyewe kwani unaweza kuitoboa kabisa ngoma ya sikio, kumbuka hata pamba maalumu zinazouzwa kwa jaili ya masikio hazikubaliki kitaalamu na ni moja ya vyanzo vya kuziba masikio.
 

Post a Comment

50 Comments

  1. Vipi mafua makali husababisha matatizo ya sikioo

    ReplyDelete
    Replies
    1. ahsante kwa swali lako zuri..!
      Kiukweli hii sio sana kutokea ila hutokea kwa baadhi ya watu kupata ugonjwa wa sikio ambao chanzo chake ilikua ni homa na mafua, mara nyingi wagonjwa wanaopata matatizo ya masikio ya aina hii huweza kupona kwa kwenda spital na kupatiwa dawa antibiotic ambayo huondoa uchafu na maji maji yalikuemo ndani ya sikio.

      Delete
  2. Naomba msaada, , mimi ni wiki ya pili sasa sikio langu moja lime. Ziba,, nime2mia dawa ya matone pia na vidonge amabvyo nilipewa zahanati , lakin bado halija zibuka, ,tatizo lina weza kuwa ni nini , mana lina nikosesha raha,,,

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pole sana, Baada ya kutumia hiyo dawa ya matone na vidonge ulirudi tena hospitali kwa uangalizi zaidi? Kama bado fika zahanati haraka iwezekanavyo.
      Kikawaida sikio likiwa limeziba huwa lina uchafu mwingi ndani au limeingia maji na wakati mwengine huwa kuna tatizo kwenye ngoma ya sikio. Kma lina uchafu unapotumia dawa ya matone baada ya siku 5 au 10 kama halijazibuka unatakiwa ukasafishwe kw kupigwa bomba ili kutoa uchafu na takataka zote zilizomo ndani ya sikio.


      Delete
  3. Habari! Mimi.nina shida ya ushauri wa dawa gani
    nitumie ili kuamsha mshipa wa sikio uliosinyaa au kukauka? ..

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nzuri..! Pole sana

      Sikio ni kiungo sensitive sana hvyo huwez kutumia dawa bila kucheki tatizo husika kwasababu matatizo mengine ya sikio dawa zake mpaka baada ya uchunguzi wa kina. Naweza kukwambia dawa ila ikaja ikakuengezea matatizoili kuepusha hayo nakushauri fika kituo cha afya cha karibu ili uweze kupata msaada zaidi wa kitibabu.

      Delete
  4. mke wangu wakati alipokua mjamzito karibu na kujifungua alikua akihisi uwasho mkali sana kwenye masikio yote mawili na akawa anajichokele kwa kijiti

    baadae ya mda akafanya vidondo ndani ya masikio yote mawili

    kisha akawa anatumia akawa anatumi dawa ya macho tongo kwa ajili ya kuponyesha hivyo vidonda lkn bahati mbaya wakati anatumia ile dawa ya macho tongo kuna siku alihisi kuwashwa na sikio akjichokonoa tena. Baadae akahisi kuziba kwa masikio

    kaenda hospital kwa ajili ya kupata tiba lkn bahati mbaya hadi sasa masikio yameziba na tumeshaenda hspitali zaidi ya moja kwa ajili ya kutumia dawa

    ndugu naomba nsaada wenu nini tufanye ilikiweza kulitibu hili sikio

    asanteni

    ReplyDelete
    Replies
    1. pole sana, inawezekana dawa aliyotumia haikua sahihi kwa matumizi ya masikio, kwa kukusaidia kwa hilo nenda hospital nyengine ambayo huduma zake ni bora zaidi akasafishwe huenda ni uchafu ndio umesababisha hilo tatizo. ahsante

      Delete
  5. Habari mm nilikua nahisi sikio kama lina upepo...hvyo nikimeza mate au kama kuvuta mafua ndipo linafunguka,nilienda hospitali nikaambiwa lina uchafu sbb yalidumu kwa muda mrefu na nilikua nahisi kama milio usiku nikilala kwa muda wa miezi 7.sasa...baada ya kusafishwa nahisi upande wa hilo sikio unakua mzito na nikiongea sauti yangu nasikia kwa ndani na pia kuna hali kama kuna kitu kinavuta kwa ndani..inakosesha raha sana hyo hali kama upepo mzito umejaa ndani..nini tatizo,naomba ushauri

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pole sana, wakati mwengine mafua hua yanasababisha ubovu wa masikio. mkusanyiko wa uchafu masikioni unapelekea kuziba kwa masikio. kitu kzuri ni kuonana na mtaalamu wa masikio ili kukusaidia zaidi.

      Delete
  6. Mimi nafanya kazi kama ambayo nakuwa natumia headphones kwa mda mrefu, na pia nikiwa na mafua masikio yangu huwa kama yameingia maji kama yameziba.. sasa nawaza tatizo ni kukaa na hzo headphone mda mrefu au ni mafua tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mafua yanasababisha masikio kuwa mazito ila utumiaji wa headphones kw mda mrefu pia hupelekea ugonjwa wa masikio. Ni vyema kutumia kwa mda mchache au km kazi yako inakulazima kutumia headphones bs hakikisha unatumia headphones zenye kuchuja mionzi ya sauti na usitumie kwa sauti ya juu. hope ukifanya hvyo utaona mabadilko. Ahsante

      Delete
  7. Habari, na tatizo na kusikia miungurumo ndani ya sikio tatizo limeanza hivi karibuni sasa n siku ya tatu nini shida naomba msaanda nifaham na athari zake ni zipi nisipochukua hatua mapema. .?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umewahi kuingia maji sikioni? mara nyingi mingurumo sikioni hutokana na kuingia maji ndani ya sikio. na kama hukuingia maji huo ni uchafu na unahitaji kusafisha masikio yako. Athari ya kutokuchukua hatua mapema inaweza pelekea kuziba kw sikio na mwishowe kupelekea uziwi

      Delete
    2. Doctor nakama sikio limeingia maji kunanamna ya kuyatoa Ila likae sawa make nasikia Kama kengele sikio moja

      Delete
  8. Mwanangu anakuwa Kama asikii vizuri na mwanzoni alitokwa na usaha nikajua ni kawaida Ila akawa analalamika maumivu sahizi anakuwa Kama asikii vizurii nifanyeje?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pole sana, kiukweli utokaji wa usaha kwenye sikio inaashiria kwamba ndani ya sikio kuna kidondo ambacho kimeoza na kinatoa uchafu au ngome ya sikio imepata hitilafu. hvyo nakushauri umpeleke kituo cha afya cha karibu kwenda kupata huduma zaidi. ukimuwahi mapema hilo tatizo litapona na litaondoka kabisa

      Delete
  9. Hiyo dawa ya matone inauzwa shilingi ngapi na je ni mzuri kwa kutibu??

    ReplyDelete
    Replies
    1. bei zake zinatofautiana na zipo aina nyingi itategemea na aina ya tatizo linalokusumbua. Ukifika duka la madawa ukimueleza muuzaji atajua akupe dawa gn kutokana na ugonjwa wako.

      Delete
  10. Habari, Masikio yang yamepata tatizo la kutosikia na sijui tatizo ni nn

    ReplyDelete
    Replies
    1. pole sana, inawezekana yameziba kutokana na uchafu au kuna tatz kwny ngoma ya sikio. Ni vzur kwenda kituo cha afya cha karibu yako ili kupata msaada zaidi wa kimatibabu

      Delete
  11. Habar, samahani mm ninatatizo ambalo limenitokea katika sikuo moja ila limesababishwa na michezo ya mtu make nilikua nimekula afu akaja mtu akaniwekea ulimi sikioni afu nilipostuka baada ya kutoa ulimi wake nikahisi maumivu afu usiku nilipolala nikahisi kama limeziba sasa nikawa nalipiga piga kama Lina mji likagoma kuzibuka afu kesho yake asubui nikahisi kama unyevu unyevu sikioni inabidi niweke namba kuitoa naona kama vitu vyeusi kama damu ilioganda inanibidi niende pharmacy nikamueleza yule pharmacist akanipatia dawa buti bado nahisi limeziba ndo nitaanza kutumia hiyo dawa ya marine inaitwa ABGENTA nitaanza kuitumia ila sioni nafuu ila tu ndo liko vile vile leo siku ya tatu natumia hiyo dawa.Naogopa sana plz naomba unisaidie labda ni dawa gani nitumie au ni madhara gani nitakua nimeyapata plz but jana nilienda laboratory nikaambiwa nitumie kwanza hiyo dawa niliopewa but sion nafuu kabisaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. pole sana, inawezekana mtikisiko tu huo umepelekea hilo tatizo ila kwa ushauri naomba nenda kituo cha afya chengine kwa msaada zaidi, sababu unaweza kwenda kituo cha afya ila doctor asigundue tatizo ni vyema kwenda kituo cha afya chengine ili upate msaada kw upande mwengine. vile vile ni mbaya kutumia dawa ya sikio bila kufanya uchunguzi kwanza.

      Delete
  12. Yaan mpaka sasa hivi linaninyima raha kabisaa limeziba sisiki vizur kabisa sijui nifanyeje au nikahisi labda ulimi ule ulidondosha mate labda ndo yalilihasili hili sikio yaan ata sielewi

    ReplyDelete
  13. Naomba ushauri mwanangu amepunguza usikivu kwa hali ya juu sana ili akusikie inabid utumie nguvu sana tena awe amekuangalia usoni nmetumia vidonge Fulani na ya kupulizia puani lakini hali inazidi kuwa mbaya tatizo inaweza kuwa nini

    ReplyDelete
  14. Naomba ushauri mwanangu amepunguza usikivu kwa hali ya juu sana ili akusikie inabid utumie nguvu sana tena awe amekuangalia usoni nmetumia vidonge Fulani na ya kupulizia puani lakini hali inazidi kuwa mbaya tatizo inaweza kuwa nini

    ReplyDelete
    Replies
    1. pole sana, inawezekana kuna uchafu ndani ya masikio yake au masikio yaliingia maji. Kitu cha muhimu mpeleke hospital ya masikio ili apate msaada zaidi maana wakati mwengine waweza tumia dawa ila isiondoe tatizo, fika kituo cha afya upate matibabu zaidi kabla tatizo halijawa kubwa

      Delete
  15. Sikio langu limeanza tu kuuma ghafla yaani ni maumivu makali Sana sijui tatizo ni Nini? Dawa gani nitumie

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pole sana, kuna sababu nyingi zinapelekea kuuma sikio kwa hafla ikiwemo kuingia maji au mafua makali pamoja uchafu wa ndani ya sikio. Usitumie dawa bila kujua tatizo la sikio, fuka kituo cha afya karibu yako ukapate maelekezo zaidi.

      Delete
  16. Habari yako? Naomba ushauri wa sikio langu leo ni siku ya 2 toka liaanze kuniuma na nimekwenda hospital tayar na Doc akanambia limeingia maji na akanipa Dawa ya matone lkn nahisi km limevimba na husababisha km Dawna isiingie vzr! Sasa naona km linaziba ss! Naomba ushaur

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pole sana, kama limeingia maji linaweza kupona na kurudi katika hali yake ya awali ila km limeanza kuvimba fika haraka kituo cha afya kwa uchunguzi zaidi, huenda kuna tatizo jengine ndani ya sikio ikiwemo vidonda

      Delete
    2. Pole sana, kama limeingia maji linaweza kupona na kurudi katika hali yake ya awali ila km limeanza kuvimba fika haraka kituo cha afya kwa uchunguzi zaidi, huenda kuna tatizo jengine ndani ya sikio ikiwemo vidonda

      Delete
  17. Naomba kuuliza hii njia ya kusafisha masikio kwa bomba , uchafu unatoka kwa nje au anavyoingiza hayo maji na uchafu unaingia ndani ?
    Na kama maji kdg tu yakiingia sikioni unahisi sikio kuziba sasa hii njia ya bomba haina madhara ?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unaposafifisha sikio kwa bomba uchafu na maji hutoka nje. Kma sikio limeingia maji kidogo tu usiende kupiga bomba nenda kituo cha afya na muelekeze docta tatizo lako atakupatia dawa ambayo itakusaidia tatizo lako.

      Delete
    2. Mimi nilienda hospital ..doctor akanisafisha kwanjia ya pamba ..na kupewa dawa na uchafu ulitoka ila hali bado ipo vilevile...sasa naweza kurudi kumweleza atumie njia ya bomba?

      Delete
  18. Masikio yangu yamekumbwa na tatizo la kutokusikia vizuri....nawakati mwengine nasikia sauti za wadudu kama nyenz...nini tatizo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pole sana, ulikua una kawaida ya kusafisha masikio yako mara kwa mara? au uliwahi kuingia maji masikioni? Tatizo kama hili mara nyingi husababishwa na homa kali ya mafua au kuingia maji kwa masikio. Kabla kutumia dawa yoyote ni vizuri kwenda kituo cha afya kwa uangalizi zaidi

      Delete
  19. Sikio langu la kulia linasikia kwa shida Sana. Mtu akiongea kwa sauti ya chini Sana Basi Ni lazima nitumie sikio la kushoto kumsikiliza sababu siwezi msikiliza kwa sikio la kulia. Ni miaka sita Sasa Nina Hali hiyo.. je nifanye kupata msaada wa kimatibabu? Asante.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pole sana, tatizo lako linaonekana ni la muda mrefu ushauri nenda kamuone specialist wa masikio katika kituo cha afya cha karibu yako.

      Delete
  20. Samahani, mm masikio yangu yote mawili yamepata shidatoka mwaka jana, yaani napata shida kuelewa sauti zinazoingia masikioni zinakuja na muungurumo na sauti ikiwa juu sana muungurumo masikioni unaongezeka hali inayonifanya nakosa flavor ya mziki wowote ama sauti yoyote, now situmii simu kuongelea au kusikiza mziki kutokana na hizo kelele zinazopelekea kutokuelewa sauti au maneno ya kwenye sauti, Tatizo linaweza kuwa ni nini? Maana kama ni dawa nimekunywa sana sijaona unafuu wowote....

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pole sana, tatizo linaonesha kma ngome ya siko imeathirika na mionz ya sauti ulizokua unasikiliza. na kitu chengine ni kutumia dawa kabla ya kuonana na daktari mtaalamu wa masikio. ushauri wangu fika kwa mtaalamu wa masikio unaweza kupata ufumbuzi wa tatizo lako

      Delete
  21. Samahan, me nilianza kuumwa homa.na mafua, sasa vile napenga mafua na sikio la kulia likafanya kama kuziba, ni wiki ya pili sasa naenda hospital napewa dawa natumia ila bado halijazibuka, na hospital daktari alinambia sikio halina uchafu, naomba unisaidie ushauri au hata dawa.
    Yan sikio limeziba kwa ndani, naskia tu tusauti flan ivi kama mluzi ambao hauishi mda wote. Japokua sikio lingine la kushoto lipo vzr.

    ReplyDelete
  22. mtaalam ,tuambie ngoma ya sikio iliyotoboka inaweza kutibika?

    ReplyDelete
  23. Habar nilikuw naomb msaada me masikio yang, kwanz kbs yalikuw na michubuko nikaend kumuon doctor akawa aniwek daw ili kukausha iyo michubuko zaid ya miez ata 8 sas lkn kabla ya kwend kumuon doctor nilikuw na2mia daw za asir za maji lkn nilivyoon ttz linazid nd nikaend kumuon doctor kwa sas michubuko imeeish kbs sihis maumivu na mpk week iliyopit niliend ten kumuon doctor akayaangalia na ikagundulik hukun ttz lolt, lkn sas njia azijafunguk yan kam kun vitu vimezib maji sio maji yan uchafu sio uchafu yani sielew kbs nilivy muelezea doctor akanipatia daw za vidong na kujipulizia puani tang nianze kutumia nina siku ya pili sas ila sihis mabadiriko yyte pia akaniambia niwe nafany mazoez ya kuziba pua na mdomo ili kilichozib kisogee pia niwe nafuna bigjii ili kulegez nina mwak sas furaha siijui kbs nawazo san, kun mda yanakuw km yanatk kuzibuk lkn yayazibuk yan km kun vitu vimegandia nakosa furaha kbs cz mishe zang zimesimam kbs cz ya masikio. Naomba ushauli wowt ule ili niufanyie kazi

    ReplyDelete
  24. habar sikio la mwanangu limeingia kijiwe na linatoa usaha

    ReplyDelete
  25. Doctor kutoka maji sikion kwa kutumia maji nijia sahihi ama ndo hovyo kabsa

    ReplyDelete
  26. Sijui langu limeziba sisikii vivuli na ninakifua na mafua je nifanyeje

    ReplyDelete
  27. Habari mwanangu hasikii vizuri nahisi ni sababu ya kipigo anaweza pata dawa

    ReplyDelete
  28. Halo kwa matibabu ya sikio kuunguruma kupiga kelele && kutoka usaha && uchafu mabonge ya damu & kutoka vidonda sikion kutokwa vipele && kuvuma upepo $$ kuingia maji && kuwasha sikio && kuuma sikio && masikio sugu yasiyo tibika hospitalin wasiliana na dokta 0676039091 tanga

    ReplyDelete
  29. Karibu upate matibabu ya masikio yanayovuma kama upepo''yanayolia kama kengere ziiiiiii, uziwi na kutoa usaha ' sikio kuuma na vidonda sikioni na uchafu pia kuwasha wasiliana na dr karimu 0676039091 tanga

    ReplyDelete

Youtube Channel Image
Hajiizo Subscribe To watch more
Subscribe