Habari

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Advertise with us here

NAFASI ZA KAZI WIZARA YA HABARI UTALII UTAMADUNI NA MICHEZO

 Image result for nafasi za kazi zanzibar
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo kama ifuatavyo:-

1. Wahudumu Daraja la III “Nafasi 2” - Pemba na “Nafasi 1” - Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari na kupata cheti cha uhudumu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Afisa Michezo Msaidizi Daraja la III “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada ya Michezo au Utawala kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. Karani Masjala Daraja la III “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Utunzaji Kumbukumbu ‘Record Management’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

4. Dereva Daraja la III “Nafasi 2” - Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari.
• Awe amepata mafunzo ya udereva kutoka katika Chuo cha mafunzo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

5. Walinzi Daraja la III “Nafasi 3” - Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari.
• Awe amepata mafunzo ya Ulinzi kutoka katika Chuo cha mafunzo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

6. Msimamizi wa Magofu Daraja la III “Nafasi 1” - Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu cheti katika fani ya ‘Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na Uhasibu’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.



7. Afisa Habari na Mawasiliano Msaidizi Daraja la III “Nafasi 3” - Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada ya Kawaida katika fani ya ‘Habari na Mawasiliano’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

8. Customer Care Daraja la III “Nafasi 1” - Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 23 Mei, 2017 wakati wa saa za kazi.

Tangazo hili pia linapatikana katika website ya TUME YA UTUMISHI ZANZIBAR

Post a Comment

0 Comments

Youtube Channel Image
Hajiizo Subscribe To watch more
Subscribe