Habari

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Advertise with us here

NJIA RAHISI KUMI ZA KUPUNGUZA TUMBO BAADA YA KUJIFUNGUA.

baada ya kujifungua wanawake wengi hujikuta bado wana matumbo makubwa yaani wakati mwingine watu wasiokujua wanaweza wakahisi bado haujazaa, lakini ukweli ni kwamba inakuchukua miezi tisa kulivimbisha tumbo hilo hivyo hata kulipunguza huchukua muda fulani.
                                                                          
kwa kawaida kizazi kinachukua wiki mbili kurudi hali yake ya kawaida lakini mafuta yaliyoko eneo la tumbo yawezi kuondoka  kirahisi kama usipochukua hatua yeyote.
                                                                    
kitu gani kinafanya mwanamke apate tumbo baada ya kujifungua?
kwa kawaida mwanamke huongezeka kilo 12 akibeba mimba hii ni kutokana na uzito wa mtoto, uzito wa  kondo la nyuma na ulaji wa chakula ambao mtoto anauhitaji sana ili kukua lakini baada ya kujifungua mama  hupunguza kilo sita tu na  kilo sita zingine hubaki kama mafuta eneo la tumbo.

inachukua muda gani hasa kwa tumbo la uzazi kuondoka?
baadhi ya wazazi huchukua siku kadhaa, baadhi huchukua miezi kulingana na bidii ya mwanamke husika ya kulitoa tumbo baada ya kujifungua.

mambo ya kuzingatia ili kuliondoa tumbo la uzazi...
nyonyesha mtoto; kunyonyesha mtoto sio kuna ongeza kinga ya mtoto tu lakini kunasababisha kuongezeka sana kwa homoni ya oxytocin ambayo inahusika na kupunguza ukubwa wa kizazi na kuzuia homoni za uzazi ambazo zinahusika na kuongeza ukubwa wa kizazi wakati mwanamke ana mimba.
wanawake wengi wa siku hizi hawanyonyeshi kwa sababu za kiurembo lakini nakwambia wengi wao huishia kua wanene sana kwa kukosa faida hii.
vaa mkanda wa tumbo; hii ni njia ya kiasili na kizamani zaidi kwani imetumika kwa miaka mingi na watu wa rangi mbalimbali duniani.
mkanda wa tumbo husaidia kuikaza misuli ya tumbo na kuongeza kasi ya kupungua kwa ukubwa wa kizazi.
ukiwa unavaa mkanda wa tumbo au unafunga kitambaa chochote hakikisha haukazi sana au kulegeza sana ili uweze kupata matokeo mazuri.
kwa matokeo mazuri zaidi, mkanda huu uvaliwe kwa  wiki nne mpaka sita baada ya kujifungua.
fanya mazoezi; mazoezi husaidia sana kupunguza tumbo la uzazi, sio lazima kufanya mazoezi mazito sana lakini unaweza kutembea, kukimbia kidogo, kuruka kamba,cardio na kadhalika, na utapata matokea mazuri sana ndani ya muda mfupi,
fanya mazoezi angalau dakika 20 mpaka 30 kwa siku hasa pale mtoto anapokua amesinzia.
kula kwa uangalifu na epuka diet kali sana; wanawake wengi hupaniki baada ya kuzaa na  huanza kufunga kula na kuruka chakula ili wapungue haraka kitu ambacho sio kizuri kwako na kwa mtoto.
kipindi hiki bado unahitaji chakula cha kutosha ili uweze kupata maziwa mengi ya kumpa mtoto, hivyo punguza sana ulaji wa vyakula vya wanga kama ugali, mihogo, wali, ndizi na acha kabisa kula wanga ambao sio muhimu kama chips, sukari, biskuti, soda,maandazi, na fast food zote.
kula zaidi vyakula vya protein kama nyama, samaki, dagaa, maharage na karanga huku ukichanganya na mboga za majani na matunda kwa wingi.
kumbuka ni vizuri kula kidogo kidogo angalau mara sita kwa siku kuliko kula milo mitatu mizito.
pumzika; ni kweli mtoto hua anasumbua sana lakini mtoto akitulia na wewe pumzika ili upate usingizi wa kutosha.
kwa hali ya kawaida kama mama hupati usingizi mwili wako unakua katika hali ambayo sio ya kawaida, hali hii huvutia mafuta katikati ya tumbo na kukufanya uendelee kua mnene.

kunywa chai ya kijani[green tea]; majani haya yamejizolea umaarufu duniani kote kwani huondoa sumu mwilini na kusaidia sana kwenye uchomaji wa chakula kwenye mwili wa binadamu.
kwa kutumia majani ya chai haya kila siku hukusaidia sana kupunguza kitambi cha uzazi.
                                                          
kunywa maji ya uvuguvugu; kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi na hata mchana ukisikia kiu, unaweza kuchanganya na limao kidogo.
maji ya uvuguvugu huongeza kasi ya uchomaji wa mafuta ya mwili kwa kuongeza joto na kuondoa nje sumu ya mwili.
massage ya mwili; massage ni muhimu sana hasa zile sehemu ambazo zinaonekana zina mafuta sana maeneo ya tumboni.
massage pia husaida metabolism  au uunguzaji wa mafuta na ni vizuri ukaikafanyika hasa baada ya mazoezi.
epuka msongo wa mawazo; msongo wa mawazo humwaga homoni aina ya cortisol kwenye damu ya mtu, homoni hiii husababisha kuchoka  na kuongezeka uzito.
hakikisha mambo yako umeyapangilia vizuri na hata kama kuna kitu unaona kinakupa mawazo sana basi usikipe nafasi, amini matatizo yapo kwa kila mtu na yataisha tu.
kula mboga za majani nyingi; mboga za majani husaidia mmengenyo wa chakula, huondoa sumu ambazo zinajikusanya kwenye utumbo mkubwa, pia zina virutubisho vingi na uzito mdogo[calories] kiasi kwamba hata ukila nyingi haziwezi kukunenepesha...hii husaidia kupunguza uzito.
                                                                        
                                                              
mwisho;hakuna uzazi rahisi, mara nyingi ukijifungua lazima uongezeke uzito..hivyo ni wajibu wako kupambana na uzito huo mpaka urudi kwenye hali yako ya kawaida.
kuendelea kua mnene baada ya kujifungua kuna madhara mengine baadae ikiwemo kisukari, shinikizo a damu, ugonjwa wa moyo na uzazi mgumu wa mimba zijazo..

Source: Siri za Afya Bora  na DR.KALEGAMYE HINYUYE MLONDO (O653095635/0769846183)

                                                              
                                         
                                                        

Post a Comment

17 Comments

  1. Habari,mkanda unafunga kwa mda gani kwa siku?(masaa mangapi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ahsante kwa swali lako zuri....Kikawaida mkanda unaweza kufunga masaa 3 hadi 4 ila itategemea na harakati zako, km mtu wa ofisini unaweza ukajifunga mda wa asubuhi wakati unaenda kazini mpaka mda utakaorudi unaufungua ili kurelax kidogo au ukiwa mama wa nyumbani funga kwa masaa yasiyopungua matatu muda wa asubuhi mchana unaufungua than jioni ukishakoga unafunga tena hadi usiku wkt wa kulala unaufungua...

      Delete
    2. Je ni sahihi kufunga mkanda hata wakat wa unakula.?

      Delete
  2. Mimi nlijifungua kwa operation na nlikaa mwezi mzima nikaanza kufunga mkanda lakini mshono unawasha sana hadi nimeacha je, inatakiwa nikae muda gn ndipo nifunge

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pole sana. Unaweza kutumia baada ya kukauka kw mshono ndani na nje, maana mshono wakati mwengine unahadaa unaweza kuona umekauka kwa nje ila kwa ndani ikawa bado haujakauka. Hivy ungesubiria japo miezi 3 au 6 ndio uanze kutumia mkanda. Kwa sasa fanya mazoezi madogo madogo ili kurejesha misuli ya tumbo bila kuathuri mshono wako.

      Delete
  3. Replies
    1. kiukweli ya mkanda siijui ila unaweza ukafika kwenye maduka wanayouza ukapata bei zake

      Delete
    2. Gharama za mkanda mara nyingi hu range kutokana na sehemu husika kuanzia 20,000 mpk 70,000

      Delete
  4. Mimi tumbo limerudi upya baada ya kujifungua MTT was kiume ninapata njaa Sana' Nikila sishibi hivyo nakula sana tofauti na kawaida hadi najishangaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. pole sana, kula sana sio tatizo ila tatizo ni aina ya vyakula unavyokula. Vyakula vya uwanga ukila kwa wingi vinasababisha tumbo pamoja na mafuta. kula matunda kwa wingi sana na pendelea kunywa maji japo glass moja kabla hujaanza kula chakula chako. Jaribu njia hii inshaallah unaweza fanikiwa

      Delete
  5. Mimi Nina miezi miwili na siku 18 tumbo langu nilifunga kwa kanga wiki mbili lakini sasa hivi linazidi kuwa likubwa sijui nifanye nini na matiti yana kuwa makubwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. angalia aina ya vyakula unavokula, jaribu kupunguza vyakula vya mafuta.

      Ukiweza kunywa maji ya mvuke asubuhi mapema kabla hujala ktu chochote na pia pendelea kunya alau glasi moja ya maji kabla ya kula mlo wako wa kila siku. hayo ni mafuta mwilini ndo yanasababisha hali hyo

      Delete
  6. Nimependa ushauri wenu Mungu awabariki

    ReplyDelete
  7. Mimi nimejifungua kawaida lkn nikawa nakunywa uji sana kwaajili ya Maziwa sasa tumbo limefumuka kua kubwa na MTT ana miez nane ukiniona utajua Nina mimba tena nimefunga mikanda lakin bado nakunywa maji ya moto lkn bado nifanye nini Mimi?

    ReplyDelete
  8. Habar mm mtoto ni mkubwa sasa miaka 4 naweza kufunga tumbo na likarud

    ReplyDelete
  9. Kwa njia asili ya kuondoa tumbo au kupunguza kitambi && matatizo ya uzazi $$ UTI sugu & pid kuondoa mikunjo ya ngozi && kuondoa chunus usoni && ugumba wasiliana na dr 0676039091 tanga

    ReplyDelete

Youtube Channel Image
Hajiizo Subscribe To watch more
Subscribe