kipindi
cha ujauzito ni moja ya vipindi vizuri sana kwa mama anayetarajia
kupata mtoto, kipindi hiki hua na shida mbalimbali ambazo husababishwa
na mabadiliko ya mama katika nyanja mbalimbali za mwili wake. kuna mambo
ambayo ukisikia mama analalamika kipindi hiki ni kawaida lakini kuna
mambo muhimu ambayo ukiyasikia kwa mama mjamzito basi lazima uchukue
hatua kama ifuatavyo.
kutokwa na damu sehemu za siri;
damu nyingi kutoka sehemu za siri miezi mitatu ya kwanza ni dalili
kwamba mimba imeharibika na kama damu hiyo inaambatana na maumivu makali
ya tumbo la chini, inawezekana mimba imetungwa nje ya kizazi, lakini
pia damu ikitoka kipindi cha miezi ya mwisho karibia na kujifungua ni
dalili kwamba kondo la nyuma au placenta imejichomoa
kwenye mfuko wa kizazi. hali hizi zinahiaji msaada wa haraka wa daktari
hasa hasa mimba iliyotungwa nje ya kizazi, matibabu ya mimba
iliyotungwa nje ya uzazi hua ni upasuaji wa haraka bila hivyo kifo huweza hutokea.
kutocheza kwa mtoto: kawaida
mtoto huanza kucheza wiki ya 16 mpaka 25, kama mda huo ukipitiliza bila
kusikia chochote au mtoto alikua ameshaanza kucheza baadae ukasikia
kimya huu ni muda muafaka wa kuwahi kuonana na daktari kwa uchunguzi zaidi na matibabu huenda mtoto amefariki au ana tatizo fulani.
kupata uchungu kabla ya wakati: wanawake
wengi hawajui tofauti ya uchungu wa kweli na ule ambao sio wa ukweli,
mfano ukisikia maumivu kwa muda, maumivu hayo hayaongezeki na hayana
muda maalumu huo sio uchungu. ila ukisikia maumivu yanayotofautiana
angalau kwa
dakika kumi na maumivu yanazidi muda unavyozidi kwenda huo ni uchungu
wa kweli. wahi hospitali ukasaidiwe kujifungua au kama muda bado nenda
hospitali ili wazuie uchungu huo ili mtoto asizaliwe kabla hajakomaa.
kupasuka kwa chupa ya uzazi;
hii kitaalamu inaitwa rapture of membrane, halii hii hutokea muda
fulani baada ya uchungu kuanza na ni kawaida, lakini ukiona maji
yanamwagika ghafla na una mimba kubwa inawezekana chupa hiyo imepasuka
hivyo kuhakikisha nenda chooni alafu kojoa mkojo wote, ukiona maji bado
yanaendelea kutoka basi maki hayo yanatoka kwenye mfuko wa uzazi hivyo
kimbilia hospitali haraka kwani mtoto yuko hatarini.
maumivu makali ya kichwa, kutoona vizuri, tumbo kuuma na kuvimba miguu; hizi
ni dalili za kifafa cha mimba, ugonjwa huu umeua wanawake wengi sana
kipindi cha kujiufungua, kuhakikisha hali hii nenda ukapimwe presha na
ukiona presha iko juu kuliko kiwango cha kawaida wahi hospitali utibiwe.
SOURCE: dr kalegamye hinyuye mlondo --->>> http://sirizaafyabora.blogspot.com/
1 Comments
Asante kwa somo
ReplyDelete