Habari

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Advertise with us here

Jinsi ya Kuishi na Vidonda vya Tumbo

vidonda-tumbo 
Kama una vidonda vya tumbo, matibabu yako yatategemea sababu ya vidonda vya tumbo. Kama ni bakteria H.pylori, dawa za kuua na kuondoa bakteria hutumiwa.
Kama ni Non-Steroidal Anti-Inflamantory Drugs 'NSAIDS' mfano Aspirin & Ibuprofen utapaswa kutumia Proton Pump Inhibitor 'PPI' mfano Omeprazole & Esomeprazole.

Ingawa matibabu ya siku hizi husisitiza kuchanganya dawa za kuua bakteria na Proton Pump Inihibitors 'PPI'.

Mambo yafuatayo yatakusaidia kuishi vizuri ukiwa na 'Vidonda Vya Tumbo':-

=> Acha kutumia kahawa na chai, kwa maana vitu hivi huongeza kiwango cha asidi kinachotengenezwa na tumbo lako. Unaweza tumia chai ya mitishamba 'Herbal tea' kama mbadala.

=> Kunywa maziwa na ule vitokanavyo na maziwa kama maziwa mgando 'Yoghurt', jibini 'Cheese'. Maziwa hufikiriwa kufunika utumbo na kupunguza athari za asidi ya tumboni.

=> Jitahidi kupunguza uzito kama uzito umezidi na hauendani na kimo chako.

=> Kula walau kidogo mara kwa mara. Hii itasaidia kupunguza athari za asidi inayotengenezwa na tumbo.

=> Acha au kunywa vileo siku maalumu tu kwa maana unywaji wa pombe mara kwa mara hutonesha kwenye vidonda vya tumbo vinavyotaka kupona.

=> Epuka matumizi ya viungo vya vyakula kwa maana hufanya hali kuwa mbaya zaidi.

=> Acha kuvuta sigara/tumbaku/bangi. Uvutaji wa sigara utakuweka kwenye hatari zaidi ya kuanza vidonda vipya na kuzuia vidonda vingine visipone.

Source: kutoka Fikra Pevu

Post a Comment

0 Comments

Youtube Channel Image
Hajiizo Subscribe To watch more
Subscribe