MUENDELEZO.......
kufuatulia mzunguko wa hedhi; mzunguko
hufuatiliwa kuangalia kama unaenda vizuri na hakuna vitu ambavyo sio
vya kawaida ambavyo ni dalili za ugumba kama kuona hedhi mara mbili kwa
mwezi, maumivu makali wakati wa hedhi, kupata damu yenye mabonge na
harufu isiyo ya kawaida.
kufuatilia joto la mwili na utando unaotoka sehemu za siri; kama huna uhakika sana na siku yako ya hatari nunua themometer ya digitali ambayo ni rahisi kusoma[inauzwa elfu kumi tu] ya kupima joto kisha pima kila asubuhi. siku zako za hatari ya kubeba mimba joto litaongezeka kwa 0.5 degree na utando huo kama wa yai bichi utatoka.
endometrial biopsy; hichi ni kipimo ambacho huchukuliwa kuangalia kama kuna tatizo lolote kwenye kuta za za kizazi. hivyo kiasi kidogo cha nyama hukatwa na kwenda kuchunguzwa.
upimaji wa kiwango cha homoni; mwili wa binadamu una homoni nyingi sana, baadhi ya homoni kama oestrogen na
progesterone huhusika moja kwa moja kwenye mfumo wa uzazi, hivyo ili
mtu aweze kubeba mimba lazima homoni hizo ziwe kwenye kiwango fulani
sahihi. yaani zisiwe kwa kiasi kikubwa sana au kidogoga sana. hivyo vipimo hivyo ni muhimu kwenye kutibu ugumba.
hysterosalpingiography;
kipimo hiki hupimwa siku saba mpaka kumi kabla yai halijashuka,
hutumika sana kuangalingalia kama mirija ya inayopitisha mayai ya uzazi
imeziba au vipi.
laparascopy; kipimo hichi hutumika kuangalia kama kizazi, mirija ya mayai na mayai yanapozaliwa kama ni pazima au vipi.
utrasound; hii ni mashine ya picha inayopatikana sehemu nyingi sana, huangalia kama kama kuna uvimbe wa kizazi, ugonjwa wa kizazi,, uvimbe wa ovari na kadhalika. ina uwezo wa kuona vitu vingi kwa wakati mmoja.
MATIBABU YA UGUMBA.
matibabu
ya ugumba ni magumu sana na yanaumiza kichwa kwani kila mtu hupatiwa
dawa kulingana na chanzo cha ugumba wake, ukisikai kuna mganga ana dawa
moja ya kutibu ugumba kwa watu wote huyo ni muongo, kimbia mbali hakuna
kitu kama hicho. kimsingi
ni kwamba mtu asipewe dawa yeyote bila kufanya vipimo na kugundua
chamzo cha tatizo lake lakini pia matibabu hayatakamilika bila mwanaume
kupimwa kujua kama ni mzima au vipi. matibabu yanaweza kua kama ifuatavyo;
weka mazingira ya kupata mimba;
yaani punguza uzito, acha kuvuta sigara, shiriki tendo la ndoa kila
siku isipokua siku ya hedhi tu kwa mwezi mmoja mfulululizo.
dawa za kusaidia kushuka mayai;
dawa kama clomiphene citrate hutumika kusaidia yai kushuka kwa wanawake
ambao hawana tatizo lolote la kiafya lakini mayai yao hayashuki kwenda
kwenye kizazi.
gonadotrophins; hii ni dawa ambayo hutumika iwapo clomiphene citrate niliyotaja hapo juu ikishindwa kusaidia kazi vizuri.
ugumba usiofahamika chanzo chake. wakati mwingine mtu anaweza kua mgumba na akapima kila kitu kikaonekana kizima, hawa hufanyiwa kitu kinaitwaa artifiacial insermination yaani mbegu za mwanaume zinaingizwa moja kwa moja kwenye mfuko wa uzazi.
mwisho: tatizo la uzazi linaweza likachukua miaka kupona na bahati nzuri kama shida yako haiwezekani, madaktari watakwambia ukweli mapema japokua waganga wa kienyeji hua sio wepesi kusema ukweli na lakini pia, dawa nilizozitaja hapo juu hutolewa tu na daktari bingwa wa uzazi baada ya kujiridhisha kwamba unazihitaji kweli.
SOURCE: dr.kalegamye >>> http://sirizaafyabora.blogspot.com
0 Comments