Utafiti wa kampuni moja ya Sweden
uliofanyiwa watu milioni 5 umeonekana kuthibitisha nadharia kwamba urefu
wa mtu na hatari za ugonjwa wa saratani zina uhusiano.
Matokeo yake yalibaini kwamba kwa kila ziada ya sentimita 10,wakati mtu anapokuwa mtu mzima hatari za kushikwa na saratani huongezeka kwa asilimia 18 miongoni mwa wanawake na asilimia 11 miongoni mwa wanaume.
Tafiti za awali zimeonyesha uhusiano kati ya urefu wa mwanadamu na hatari za kushikwa na ugonjwa wa saratani,ijapokuwa haijulikani ni kwa nini.
Ripoti za awali za utafiti huo zilizowasilishwa katika mkutano wa wagonjwa wa watoto,watafiti kutoka taasisi ya Karolinska mjini Stockholm walielezea vile walivyolifuatilia kundi moja la watu wazima kwa zaidi ya miaka 50.
Wanawake warefu wana hatari kubwa ya hadi asilimia 20 ya kupatikana na
saratani ya matiti huku wanaume na wanawake warefu wakiwa na hatari ya
juu ya kupatikana na saratani ya ngozi kwa asilimia 30.
UNA MAONI GANI JUU YA HILI?
SOURCE: http://www.bbc.com/swahili
0 Comments