Mtu wangu wa nguvu kama bado hujakutana
na list ya zinazotajwa kuwa simu zenye thamani zaidi duniani, mtu wako
wa nguvu nimekutana nayo list hiyo, mara nyingi tumezoea kuona na
kusikia mtu akinunua simu kwa gharama ya juu huenda ikawa ni kati ya Tsh
milioni 1 hadi milioni mbili, ila hii ni TOP 5 ya simu kali na zenye
thama duniani
5- Diamond Crypto Smartphone
Hii ni moja kati ya simu zenye gharama
zaidi duniani, sio kwa sababu imetengengenezwa kwa material yenye
thamani, ila hata teknolojia iliyotumika kutengenezea sio ya kawaida, ni
ya kitalaam sana, pia inatajwa kuwekewa security ya information, simu
imepambwa kwa dhahabu na almasi katika baadhi ya maeneo. Bei yake
inatajwa kuwa dola milioni 1.3 ambazo ni zaidi ya bilioni 2 za kibongo.
4- GoldVish Le Million
Imetengenezwa na kubuniwa na
dezaina Emmanuel Gueit na kuzinduliwa Switzerland, imetengenezwa kwa
material ya dhahabu na almasi pia, hii hupatikana kwa oda huwezi
kuikutan ikiuzwa dukani, mwaka 2006 moja kati ya wafanyabiashara wa
kirusi aliinunua simu hii kwa euro milioni 1 zaidi ya bilioni 2 za
kitanzanina kuweka rekodi ya kuwa simu ghali zaidi duniani kwa wakati
huo.
3- IPhone 3G King’s Button
Hii ni moja kati ya simu zinazotajwa
katika list hii, home button yake tu imenakshiwa kwa madini ya almasi,
lakini madini ya dhahabu yapo pia katika simu hiyo, bei yake inatajwa
kuwa kati ya dola milioni 1.5 hadi dola milioni 2 zaidi ya bilioni 4 za
kibongo.
2- Supreme Goldstriker IPhone 3G 32GB
Simu hii imebuniwa na Stuart Hughes na
ipo nafasi ya pili katika list ya simu zenye thamani zaidi duniani kwa
mwaka 2015/2016. Bei yake inatajwa kufikia dola milioni 3.2, ambazo ni
zaidi ya Tsh bilion 7.
1- Diamond Rose IPhone 4 32GB
Kampuni ya Stuart Hughes imebuni pia na simu yenye thamani kuliko zote duniani Diamond Rose IPhone 4 32GB, material
ya madini ya dhahabu na almasi yote yametumika kutengeneza simu hii,
ila inatajwa kutengenezwa kwa teknolojia ya juu zaidi. Bei yake
inafaikia dola milioni 8, ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 17.
Post hii ni original kutoka website ya millardayo
2 Comments
asante kiongozi kwa somo yangu haipo katiks list japo bei mbaya
ReplyDeleteha ha ha next time itakuepo
Delete