Lengo kuu la kuanzishwa Taasisi ya Viwango ya Zanzibar ni kuhakikisha kuwa Zanzibar inakua na viwango kwa ajili ya bidhaa na huduma na kusimamia ubora wa bidhaa na huduma hizo. Viwango na bidhaa zenye ubora zinalenga kulinda afya na usalama wa watumiaji pamoja na kukuza uchumi wa Zanzibar na kuhifadhi mazingira ya nchi.
Taasisi ya Viwango ya Zanzibar (ZBS) inakaribisha maombi ya kujaza nafasi tupu katika kada mbali mbali kwa waombaji wenye sifa stahili katika Ofisi yake iliyopo Unguja na Pemba.
Nafasi zenyewe ni kama zifuatazo:-
UNGUJA
1. AFISA UDHIBITI UBORA NA UKAGUZI DARAJA LA II – Nafasi moja
Sifa za muombaji:
- Awe na elimu ya Shahada ya kwanza au Stashahada ya juu au Stashahada ya uzamili ya sayansi ya kemia, fizikia au sayansi ya mazingira kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
- Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
- Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.
Sifa za muombaji:
- Awe na elimu ya Shahada ya kwanza au Stashahada ya juu au Stashahada ya Uzamili katika fani ya Uchumi (Economics), Mipango (Planning), Uongozi wa Biashara (Business Administration) au fani inayolingana kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
- Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
- Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.
Sifa za muombaji:
- Awe na elimu ya Shahada ya kwanza au Stashahada ya juu au Stashahada ya uzamili ya sayansi ya kemia, uhandisi majengo (Civil engineering), vipimo (metrology), petroli na gesi au fani inayolingana kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
- Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
- Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.
Sifa za muombaji:
- Awe na elimu ya Shahada ya Kwanza au Stashahada ya juu au Stashahada ya Uzamili ya Ugavi na Ununuzi (Procument and Supply) au fani inayolingana kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
- Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
- Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.
Sifa za muombaji:
- Awe na elimu ya Shahada ya kwanza au Stashahada ya juu au Stashahada Uzamili ya Uhandisi Majengo (Civil engineering) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
- Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
- Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.
6. AFISA UDHIBITI UBORA NA UKAGUZI DARAJA LA II – Nafasi moja
Sifa za muombaji
- Awe na elimu ya Shahada ya kwanza au Stashahada ya juu au Stashahada ya uzamili ya sayansi ya kemia, fizikia au sayansi ya mazingira kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
- Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
- Awe mkaazi wa Pemba.
- Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.
Muombaji anatakiwa aandike barua ya maombi na kuambatanisha na barua hiyo:
a) Vivuli vya vyeti vya kumalizia masomo.
b) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
c) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
d) Picha mbili za Muombaji (Passport size).
e) Majina na anuani za Wadhamini wawili wanaotambulika.
f) Anuani rasmi anayopatikana muombaji, barua pepe na nambari ya simu.
Muombaji anatakiwa aainishe nafasi moja anayoiomba kati ya
zilizotajwa hapo juu vinginevyo maombi yake hayatazingatiwa. Muombaji
yeyote atakayeomba nafasi zaidi ya moja maombi yake hayatozingatiwa.Maombi yote yatumwe kwa anuani ifuatayo:-
MKURUGENZI MKUU,
TAASISI YA VIWANGO YA ZANZIBAR,
S.L.B 1136,
ZANZIBAR.
Barua za maombi ziandikwe kwa mkono na ziwasilishwe moja kwa moja Ofisi ya Taasisi ya Viwango Zanzibar iliyopo Eneo la Viwanda Amani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao katika Ofisi ya Taasisi ya Viwango Zanzibar iliyopo Chake Chake Pemba.
Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni siku ya Alkhamis tarehe 4 Mei 2017, saa 9.30 alaasiri.
Mawasiliano yatafanywa kwa wale tu watakaopita katika mchujo wa awali (short listed).
Tangazo hili linapatikana pia katika Tovuti ya Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) ambayo ni www.zbs.go.tz.
0 Comments