Ukiulizwa swali hili Mara nyingi kwa kulijibu kwa swali hili
utapata shida sana. Kwa sababu huwezi kuja na jibu moja ndo ukasema
sababu hii ndiyo imesababisha Waafrika wengi kuwa maskini. Kuanzia miaka
ya 1960 na kuendelea jibu kwa wengi hasa magwiji wa Historia na
Wanaharakati maarufu wa kiafrika na waliokuwa nje ya Afrika walikuwa
wanakuja na jibu MOJA TU, nalo ni ukoloni. Ukoloni kwa sababu ulinyonya
rasilimali nyingi sana za kiafrika. Pia walifanikiwa kuwahadaa Waafrika
na elimu isiyoendana na mazingira yao wakaja kuwa watumwa kifkira. Kuwa
watumwa kifkira likatokea tatizo sugu sana ambao nalo ni mwendelezo mwa
sababu ya kwanza ya umaskini wa Waafrika ambalo ni UKOLONI MAMBO LEO.
Nakubaliana na sababu ya ukoloni ambao umezaa ukoloni mamboleo kuwa ni msingi wa umaskini mkubwa wa bara la Afrika. Mwalimu Nyerere kabla hajaondoka duniani alisema kuwa,nchi za afrika zilipopata uhuru viongozi wake walikuwa na maono na mikakati madhubuti kabisa ya kupambana na ukoloni mamboleo pamoja na umaskini. Kizazi kilichofuata kilikuja kulegalega na kwa sababu Kilianza kuzidiwa na ukoloni mambo leo, kwa kifupi Nyerere alisema kilianza kukosa dira kabisa. Na akawa na matumaini kwa kusema anaona Afrika mpya, Afrika ambavyo watu wengi watakuwa wanaishi maisha mazuri, Afrika ambayo itaweza kutoa mnyororo wa ukoloni mambo leo. Lakini Mwalimu Hatuko naye kwa sasa, bila shaka angekuwepo angetupa jibu zuri kwa hali iliyopo Afrika.
Tatizo kubwa kwa sasa katika nchi za kiafrika ni Uzalendo. Mfano, katika halimashauri zetu hapa Tanzania au taasisi nyingi tu,utakuta mtu akiajiliwa anakuwa na maono mazuri ya kimaendeleo. Tatizo akifika ofisini anakutana na mifumo miwili. Mfumo halali ndani ya sehemu alipo na mfumo ulioota mizizi na umekuwa kama ndo mfumo halali kabisa,nao ni mfumo wa kutotoa huduma vizuri kwa wateja, kutofanya kazi ipasavyo mpaka mtu a pâté chochote ndiyo afanye au ahudumie watu wake. Na mbaya zaidi viongozi wanaotakiwa kukemea ndiyo wanaofanya hayo. Utakuta maono yako yako kinyume kabisa na watu wengi,hapo ndipo wazalendo wachache wanapozidiwa na majambazi wakubwa wa rasilimali za afrika.
Uzalendo ninavyouchukulia binafsi,kama wewe ni mfanyakazi wa nyumbani na unalipwa fanya kazi ipasanyo,kama wewe ni mkulima fanya kazi, kama wewe ni Mwalimu fanya kazi ipasavyo,kama wewe daktari timiza wajibu wako. Kama wewe raisi wa nchi waonee huruma wananchi wako timiza wajibu wako ipasavyo.
Tatizo kubwa la Afrika ni Waafrika wengi wamepoteza uzalendo kabisa. Kwa niñi limetokea hili?. Tufanye nini kuweza kurudisha uzalendo ili angalau turudi kwenye msingi?
Au tumekuwa tukichagua viongozi hawa hapa wafuatao kama Plato Myunani wa kale alivyonena. Yeye alisema kuwa viongozi wanaofaa kutuongoza ni;
a) Wanafalsafa
-Hawa wana sifa mbili muhimu, sifa ya kwanza; Wanaweza kuongoza, ya pili hawapendi kuongoza. Hawa Plato alisema ni vizuri waongoze maana hata kung'ang'ania uongozi hawataki, maana miaka yao ikiisha waliochaguliwa watafurahi maana watarudi kwenye kazi zao za falsafa. Hawa Nyerere kwenye kitabu chake cha Viongozi wetu na Hatma ya Tanzania aliyesema a nadhani kwa Tanzania hawa hawapo kwa sasa.
b) Wanaopenda kuongoza na hawana uwezo wa kuongoza.
-Hawa watu nao Wana sifa zao; kwanza, wanapenda kuingia kwenye madaraka kwa njia zozote chafu maana njia halali ni vigumu kuchaguliwa na watu. Wanaingia kwa kutumia rushwa, vitisho, kuua,udanganyifu mwingi. Hawa watu wakishaingia madarani maana hawajui Hatma Yao Mara nyingi utawala wao wanaulinda wa njia yoyote ile chafu. Wanna fanya hivi maana hata wakitoka huwa hawajui watafanya kazi gani?.Wakitoka nani atawatetea kwa dhuruma walizofanya?. Hawa ndo wako wengi katika bara la Afrika. Na wameota mizizi Afrika maana wamezagaa kila koan ya Afrika na jeshi Lao ni kubwa mno. Na hawa viongozi wengi tulio nao kuanzia ngazi za chini mpaka juu. Ukiwasikiliza matamshinyao utafhani Wanauchungu na bara la Afrika. Na hawa ndo wanachangia bara la Afrika kuwa maskini.
c) Viongozi wanaojua uongozi ni WAJIBU.
-Hawa ukiwapa uongozi wanajua kabisa uongozi ni wajibu na wajibu ni kufanya kazi tu. Hawa binafsi nawachukulia kuwa wanaamini katika kufanya kazi ili mtu upate haki yako. Hawa ukiwachagua nao wanasifa zao, sifa Yao kubwa ni kwa sababu anajua uongozi ni wajibu, atafanya kazi sana ili aweze kutimiza wajibu wake. Na asipouyimiza huwa anaumia sana moyoni na Mara nyingi atawaambieni kwa niñi ameshindwa kutimiza wajibu aliokuwa amejiwekea. Hawa tunao wachache sana Afrika na Mara nyingi wanazidiwa na kundi la pili maana kundi la pili Lina jeshi kuwa sana. Na hili kundi huwa haling'ang'anii katika madaraka kama kundi la pili, maana wanaingia kwenye uongozi kwa njia halali na wanapenda kutoka kwa njia hizohizo. Hili ndo kundi ambalo linatakiwa kwa nchi zetu za Afrika ili liweze kupunguzankwa kasi kuwa umaskini.

Tupe maoni yako juu hili...mchango wako ni muhimu sana kwetu na kwa wengine!!
0 Comments