Habari

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Advertise with us here

NEWS UPDATE - SIASA...MICHEZO #MAGAZETINI

MWANANCHI
Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) limekubaliana na ombi la klabu za Ligi Kuu la kusajili wachezaji saba wa kigeni badala ya watano wa sasa.
Bodi ya Ligi iliwasilisha uamuzi wa klabu zote za Ligi Kuu wa kuiomba TFF ibadilishe kanuni ili ziweze kusajili wachezaji wengi zaidi wa kigeni kwa lengo la kuinua kiwango cha ligi hiyo.
Jana, katibu mkuu wa TFF, Celestine Mwesiga alisema kikao hicho cha shirikisho hilo na sasa klabu zinaweza kusajili wachezaji zaidi wa kigeni.
Klabu hizo zimekuwa zikijikuta kwenye wakati mgumu kuamua kukata jina la mchezaji wakati zinapokuwa na wachezaji wengi wazuri kutoka nje, ikiwamo Yanga ambayo hadi sasa ina wachezaji sita wageni na ilikuwa ikisubiri uamuzi huo ili ikamilishe usajili wa wachezaji wageni.
Wakati hayo yakiendelea, Yanga imemruhusu kipa wake Juma Kaseja kusajiliwa na klabu yoyote inayomhitaji.
Mwanasheria wa Yanga, Frank Chacha aliliambia gazeti hili jana kuwa Yanga haiwezi kumzuia kipa huyo kujiunga na klabu nyingine yoyote kwa kuwa tayari ilishavunja mkataba wake, hivyo siyo mwajiriwa tena wa klabu hiyo yenye makao yake makuu makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani.
Timu mbalimbali za Ligi Kuu zilielezwa kuwa zimekuwa zikihitaji huduma ya kipa huyo aliyejipatia sifa kwa umahiri langoni, kiasi cha kujipatia jina la Tanzania One, lakini zilikuwa zikihofia kesi yake ya kimkataba dhidi ya Yanga iliyopo Tume ya Usuluhishi ya Mahakama ya Kazi.
Kaseja alisaini Yanga mkataba wa miaka miwili na alitumikia mwaka mmoja na kubakisha mkataba wa mwaka mmoja uliozua mgogoro.
Chacha alisema anashangazwa na watu wanaodaia kuwa klabu hiyo imemzuia Kaseja kujiunga na timu yoyote wakati si kweli.


“Sisi hatumzuii Kaseja kujiunga na timu yoyote na hata mwanasheria wake tulimwambia hivyo kuwa anaweza kutafuta timu wakati kesi yake inaendelea.
“Ndiyo ana kesi na Yanga, lakini kumbuka yeye ndiye alivunja mkataba na Yanga ikamshtaki hivyo haitapendeza kuwa hukumu inatoka halafu Kaseja hana timu yoyote inayomwingizia kipato, atailipa nini Yanga.
Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu jambo hilo, Kaseja alijibu kuwa hawezi kulizungumzia kwa sasa.

MWANANCHI
Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amewashangaa makada wanaojinadi kuwa ni wasafi na waadilifu, akisema sifa hizo zinatakiwa zitolewe na jamii.
Jaji Warioba, mmoja wa watu ambao wamekuwa wakikemea masuala ya ukiukwaji wa maadili, pia amesema hatamuunga mkono mgombea ambaye anakiuka maadili ya uongozi.
Tayari makada 37 wamejitokeza kuomba ridhaa ya wana-CCM kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na wengi wao wamekuwa wakijinadi kuwa ni wasafi na waadilifu na kuwataka wanachama kutowapitisha watu wenye harufu ya ufisadi na wasio waadilifu.
Lakini Jaji Warioba alisema anaona wanakwenda kinyume na inavyotakiwa kufanyika.

“Viongozi wa sasa wanaonekana hawajali misingi ya maadili kwa sababu jamii yetu yenyewe imeonyesha kutochukizwa na suala hili la mmomonyoko wa maadili na wala jamii haijalipa uzito unaostahili,” alisema Jaji Warioba wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Vuguvugu la uhuishaji wa Maadili kwa Jamii (Moral Rivival Movement).

“Viongozi wengi waliochukua fomu za kugombea urais wanaonekana kujitangaza kuwa wao ni waadilifu. Jamii ndiyo ilipaswa kusema kuwa viongozi hao ni waadilifu au sio waadilifu na sio wao kujinadi,” alisema Warioba ambaye pia aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu.

Mkutano huo ulioandaliwa na viongozi wa dini kwa kushirikiana na Chama cha Wataalamu wa Wakikristo (CPT) ulijadili ujenzi mpya wa maadili katika jamii utasadia kupata kiongozi mwenye misingi ya maadili ili kuepuka mitafaruku baina ya siasa za madaraka na siasa za maslahi.
Warioba, ambaye alieleza kuwa ameamua kukaa kimya kuhofia kila anachosema kuhusishwa na masuala ya uchaguzi, alisema viongozi ambao hawana maadili wamechangia kwa kiasi kikubwa kuwapo kwa mianya ya rushwa.

“Lakini kama tunataka kuwa na viongozi wenye misingi ya maadili, ni lazima tujenge upya maadili kwa sababu tusipofanya hivyo yatazidi kuporomoka,” alisema waziri mkuu huyo wa zamani.
“Tumeona sasa ukabili umeanza kurudi, ubaguzi wa kidini umeanza kurudi, ubaguzi wa kikanda umeanza kurudi, ubaguzi wa namna hii umeanza kurudi kutokana na kukosekana kwa maadili,” alisema Jaji Warioba ambaye alitumia muda mwingi kuishauri jamii kufuata misingi ya maadili iliyoachwa na waasisi.

MWANANCHI
Serikali imesema kuanzia Julai mosi mwaka huu, ajira za utumishi wa umma zitakuwa zikiombwa kwa njia ya mtandao, ili kuongeza ufanisi wa mchakato wa kuwapata watumishi wenye sifa na kupunguza malalamiko ya kupotea kwa barua za maombi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi), Celina Kombani alisema mtandao huo umezinduliwa na waombaji watapaswa kuingia katika tovuti maalumu ya ajira na kutuma maombi yaliyoambatanishwa na vyeti vya taaluma walizosomea.

“Maombi kwa njia ya mtandao yatapunguza kazi ya kuchambua maelfu ya barua za maombi ya kazi zilizokuwa zinatumwa, itapunguza pia manung’uniko kwamba barua zimetumwa kisha zimekaliwa tu,”  Kombani.

Waziri huyo, alisema kwa kutumia utaratibu huo mpya, wananchi wanaotaka ajira serikalini watakuwa na uhakika kuwa barua zao zimefika na kupokewa na wahusika. Pia, wanaweza kupata mrejesho kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu zao za mkononi.
Kwa upande wake Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Xavier Daudi alisema baada ya kuona mchakato wa kuajiri unachangamoto nyingi, waliamua kubuni mfumo wa kuomba ajira kupitia mtandaoni.

“Utaratibu huu utatupunguzia gharama, wanafunzi wanaohitimu kila mwaka vyuoni ni maelfu kwa maelfu na nafasi tunazopata serikalini kupitia sekretarieti ya ajira hazizidi 12,000 kila mwaka,” Daudi.
Hata hivyo, katibu huyo alisema wamekuwa wakipata changamoto kubwa kutokana na baadhi ya waombaji kutumia vyeti vya kughushi na hivyo kulazimika kwenda kwenye vyuo husika kuvithibitisha.

MWANANCHI
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kinazindua operesheni mpya ya kuwaandaa wanawake kufanya “maamuzi magumu” kwenye Uchaguzi Mkuu ujao.
Kwa sasa, chama hicho kikuu cha upinzani, kinaendelea na kampeni ya “Amsha Amsha”, ambayo inalenga kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la Wapigakura.
Jana, Chadema ilitoa taarifa inayoeleza kuwa sambamba na kampeni hiyo ya Amsha, Amsha”, chama hicho kinaanza operesheni mpya itakayozinduliwa na katibu wake mkuu, Dk Willibrod Slaa huku wanamuziki nyota, Christian Bella, Profesa Jay na Flora Mbasha wakipamba uzinduzi huo.
Mratibu wa operesheni hiyo, Lilian Wasira alisema jana kuwa shughuli hiyo itafanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam.

“Maandalizi yamekamilika, wanawake Dar es Salaam na Pwani waje wajengeke kifikra ili kufanya maamuzi magumu katika uchaguzi unaokuja,” Wasira.

Alisema operesheni hiyo itafanyika nchi nzima kuhamasisha wanawake kujiandikisha kwenye Daftari ya Wapigakura na kuwapa elimu ili watambue nafasi yao katika jamii na uwezo wao kuleta maendeleo ya kweli,” alisema Wasira.
Kada huyo, aliyewania uenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema bila mafanikio, alisema: “Zama za wanawake kupewa khanga, vitenge, vilemba na kofia wakati wa uchaguzi zimepitwa na wakati, lazima wajithamini, ndiyo maana tumeanzisha hii operesheni ili tuwajenge kiuwezo.”
Alisema ni wakati mwafaka kuachana na fikra za kurubuniwa na kuuza haki zao za msingi kwa rushwa za aina mbalimbali kama “chumvi”, akishauri watambue kuwa njia pekee ya kuiondoa CCM madarakani ni kujiandikisha katika Daftari la Wapigakura na kugombea uongozi.

“Hatutaki kuona hali ikiendelea. Saa ya ukombozi imefika, mwanamke amekuwa ni mwathirika wa matatizo mbalimbali kwenye jamii, hivyo asiache kuja kesho (leo) ili Tanzania izaliwe upya Oktoba,”  Wasira.

Mbali na Dk Slaa, hafla hiyo itahudhuriwa na mbunge wa Kawe, Halima Mdee na wasanii wa muziki, wote wakiwa na lengo la kutoa hamasa kwa wanawake nchini kushiriki katika siasa. Ikiwa ni miezi minne imesalia kabla ya uchaguzi wa Oktoba, Chadema imesambaza makada wake walio kwenye mabaraza ya wanawake na vijana kwenda maeneo mbalimbali kuhamasisha uandikishaji wapiga kura.
Juzi gazeti hili lilimkariri mkurugenzi wa mafunzo na uchaguzi wa Chadema, Benson Kigaila akisema kwa sasa wanaelekeza nguvu katika uandikishaji wa wapigakura ili kutengeneza mazingira mazuri ya ushindi.
Hamasa hiyo inakwenda sambamba na mchakato wa kuchukua na kurudisha fomu, ikiwa ni siku saba kabla ya siku ya mwisho ya hatua hiyo kwa watiania wa ubunge na udiwani katika maeneo yasiyo na uwakilishi wa madiwani na wabunge.

MTANZANIA
Mbunge wa Sengerema Willium Ngeleja amesema iwapo CCM kitamteua kuwa mgombea wa Urais katika uchaguzi mkuu utakaofantyika Oktoba na kuibuka mshindi Serikali atakayiiunda haitakumbatia ushoga wala ndoa za jinsia moja.
Ngeleja aliyasema hayo wakati akiwashukuru wananchi wa Nyamagana kwa kumdhamini ili kutimiza mat akwa ya chama chake ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea wa Urais.

Nikibahatika kuingia ikulu, sitakuwa naanza upya, tayari Serikali yetu chini ya Rais Kikwete imeweka msimamo juu ya suala hilo, na mimi nikiwa rais mwadilifu ninayeheshimu mila zetu njema, masuala ya ushoga hauyatakuwa nan a nafasi kabisaNgeleja.

Alisema ili kulinda utamaduni na heshima ya Kitanzania na Afrika ni muhimu kwa Taifa kuanza kuchukua hatua kupunguza utegemezi ili kuepukana na masharti ya kufedhehesha kama hayo.

MTANZANIA
Wakati idadi ya makada wa CCM waliochukua fomu ikifikia 38 jana, UKAWA wanajipanga  kumkabili LOWASSA .
Ukawa inamuona Lowassa kama ndiye mgombea kutoka CCM  ambaye ndiye wanaweza kukabiliana naye katika uchaguzi mkuu ujao kutokana na jina lake kuvuma sana hasa wakati huu mwana siasa huyo pamoja na makada wengine wa CCM wakizungumza Mikoani kuomba udhamini.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbowe alisema wanamsubiri kwa hamu Lowassa katika kinyang’anyiro cha Urais katika uchaguzi wa mwaka huu.
Katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja wa njoro, Moshi, Mbowe aliwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wapigakura pamoja na kufanya mabadiliko katika uchaguzi mkuu ujao.
Amesema ameona watu wengi wakimpamba Lowassa ambaye ametangaza nia ya kugombea Urais kupitia CCM, hivyo wanansubiri amalize michakato yote kwenye chama chake aje kukutana na Ukawa.

NIPASHE
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe, amesema utitiri wa wagombea urais kupitia CCM kunaonyesha dalili ya wao wenyewe kutoaminiana, kutothaminiana na kimepoteza hazina ya viongozi.
Aidha, alisema kazi ya urais ingekuwa inachukuliwa kwa uzito wagombea wa CCM wasingefikia 10 badala yake imeonekana ni kazi nyepesi na imerahisishwa na CCM. Kabwe alisema sifa 13 pekee za wagombea wa CCM ni nyepesi ndio maana kila mmoja anajiona anaweza kuwa kiongozi wa nchi.
Kabwe alisema moja ya sifa ya chama cha ACT-Wazalendo ni wagombea kufuata masharti kwa kutangaza mali na madeni ikiwamo kufuata miiko ya viongozi iliyotangazwa na Azimio la Tabora.
Kabwe aliwataja viongozi hao kuwa ni wa kitaifa wa chama, rais, mawaziri, wabunge na madiwani watakaotokana na chama hicho.
Aliongeza kuwa ili kubomoa mfumo wa kinyonyaji na kifisadi miongoni mwa viongozi, chama hicho kimeamua kurejesha miiko ya uongozi na kuishia ambayo imehusishwa kutokana na Azimio la Arusha.

“Chama kinamtaka kiongozi katika uongozi wa umma asiwe mkurugenzi katika kampuni au shirika la umma, awe wazi na vyanzo vyake vya mapato, mali alizonazo kwa kuzingatia utaratibu wa sheria ya nchi na kanuni za mwenendo na maadili ya viongozi,” Kabwe.

Pia, alisema kiongozi anatakiwa asiwe mfanyabiashara wa aina yoyote katika chama na serikali anapokuwa kwenye nafasi ya uongozi.
Alisema tangu wagombea hao waanze kutangaza nia hakuna mgombea urais aliyetamka neno miiko isipokuwa Samuel Sitta pekee, licha ya kuahidi kupambana na rushwa pamoja na ufisadi.

“Nitolee mfano nchi ya Canada, Uingereza, Marekani wana miiko lakini Tanzania tunageuza uongozi kuwa kichaka cha wezi kwa kutupa miiko pembeni,”Kabwe.

NIPASHE
Balozi Patrick Chokala, amekuwa mwandishi wa habari wa pili kati ya makada 38, waliojitosa katika kinyang’anyiro cha kuomba ridhaa ya CCM kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu.
Mwandishi wa habari wa kwanza kujitosa katika kinyang’anyiro hicho ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe.
Hii ni mara ya pili kwa Chokala kuwania nafasi hiyo, baada ya kujitosa mwaka 2005 akiwa Balozi wa Tanzania nchini Moscow na kushindwa kupenya, huku akija na kaulimbiu ya ‘Kiatu kwanza Benzi baadaye’, akiwa na maana ya watu wa chini kuwezeshwa kwanza matajiri baadaye.
Chokala alisema pamoja na Ilani ya CCM, ataweka mkazo wa usafiri wa reli huku akiitaja reli ya kati kuwa ya kwanza kutumia umeme.
Balozi Chokala ambaye alitumia muda mwingi kueleza nchi alizowahi kuishi na kufanya kazi ikiwamo Urusi, alisema Tanzania inahitaji rais safi katika suala la rushwa, ambaye hana tamaa, mwenye haki, msimamo, ambaye hataangalia ndugu yake akifika Ikulu kufanya mambo yasiyofaa kwani atamfukuza.

Hatuishi duniani miaka 100, unapokuwa Ikulu, uwe na msimamo wa kusaidia Ikulu…mimi simzungumzii yoyote bali nazungumzia principle,(kanuni, maadili) mimi ni mwanafunzi wa Political Science, uongozi na tabia ya nchi inategemea na kiongozi aliye juu ni kama nyumba ya msonge inategemea nani yupo juu,” alibainisha.

Aidha, alitoa mfano wa rais anaagiza Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kumpa Sh. bilioni 2, lakini naye atachota nyingi zaidi, Waziri wa Fedha na wengine watachukua zaidi, ikiwamo kutumia mbinu mbalimbali.
Balozi huyo ambaye amekuwa Mwandishi wa Rais, Ali Hassan Mwinyi, kwa miaka kumi na Rais Benjamini kwa miaka mitatu, alisema anaamini kuwa anaweza kuwa rais wa nchi kwa kuwa ana uzoefu wa kutosha ndani na nje ya nchi.

SOURCE: millardayo.com

Usisahau kutoa maoni yako hapa chini

Post a Comment

0 Comments

Youtube Channel Image
Hajiizo Subscribe To watch more
Subscribe