Habari

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Advertise with us here

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI WIZARA YA ARDHI, MAJI, NISHATI NA MAZINGIRA - PEMBA

Image result for nafasi za kazi 
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira - Pemba kama ifuatavyo:-

1. Karani Masjala Daraja la III “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya ‘Mtunza Kumbukumbu’ (Record Management) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Taarish Daraja la III “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya IV na kufaulu.

3. Afisa Utumishi Msaidizi Daraja la III “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya ‘Rasilimali Watu’ (Human Resource Management) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

4. Afisa Mipango Miji Daraja la II “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Urban and Rural Planning’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

5. Karani Mahkama Daraja la III “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya ‘Sheria’ (Law Public Administration) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 19 Mei. 2017 wakati wa saa za kazi.

Source: www.lps.go.tz

Post a Comment

0 Comments

Youtube Channel Image
Hajiizo Subscribe To watch more
Subscribe