Habari

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Advertise with us here

FAHAMU NJIA ZINAZOTUMIKA KUPUNGUZA UKUBWA WA MATITI

kawaida matiti huanza kutokea na kukua pale mwanamke anapokua amevunja ungo, ukubwa huu husabishwa na kuanza kumwagika kwa kiasi kikubwa cha homoni za uzazi yaani oestrogen, kuongezeka na kupungua kwa matiti hutegemea sana kiasi cha homoni kinachopanda na kushuka kila siku kwenye mwili wa mwanamke ndio maana kuna tofauti kidogo ya ukubwa wa matiti siku za kawaida za mwanamke na kipindi cha hedhi.
                                                          
hivyo sababu kuu za mwanamke kua na matiti makubwa inaweza kua homoni, unene, kurithi kwenye ukoo, ujauzito, kunyonyesha na matumizi ya dawa mbalimbali hasa za uzazi wa mpango.
matiti yakiwa makubwa sana humnyima mwanamke raha kabisa na hupata matatizo ya kisaikolojia hasa anaposhindwa kuvaa nguo nzuri na kukosa ujasiri mbele za watu,upele na fangasi chini ya matiti, maumivu ya mgongo, maumivu ya shingo na kupumua kwa shida wakati wa kulala.
sasa unapoamua kupunguza ukubwa wa matiti kuna njia mbalimbali hutumika kuyapunguza matiti kama ifuatavyo...

upasuaji; hii ndio njia ya haraka ya kupunguza matiti na ni salama sana kama ikifanyika na daktari mzoefu wa hizi kazi...kwa nchi ambazo zimeendelea pasuaji hizi zinapatikana sana na zaidi ya 99% ya wanawake waliofanyiwa waliridhika na matokeo.
upasuaji huu hufanyika kwa kupasua matiti na kuondoa sehemu kubwa ya mafuta  inayopatikana kwenye matiti kisha chuchu hukatwa vizuri na kuwekwa sehemu mpya ili iandene na matiti mapya, changamoto kubwa ya upasuaji huu ni gharama na haipatikani hapa nchini.
                                                               

mazoezi; ukiwa na matiti makubwa hakikisha uko kwenye uzito sahihi kwani kama wewe ni mnene basi unene wako pia unachangia kwenye ukubwa wa matiti yako, hivyo anza mazoezi ya mwili mzika kama kukimbia, kuendesha baiskeli, fanya mazoezi ya aerobics[hufanyika kwa mziki kwenye gym mbalimbali].ukianza kupungua uzito basi sehemu kubwa ya matiti yako pia itapungua ukubwa uzito. kumbuka kuvaa sidiria inayobana sana wakati wa mazoezi ili usisumbuke.



massage; kwa kutumia njia hii hakikisha kila titi unalipa muda sawa wa kulifanyia masaji ili yote yaweze kupata matokeo sahihi, chukua mafuta ya olive oil mwaga kidogo kwenye titi na uanze kulifanyaia masaji kwanzia katikati huku unazunguka kama duara mpaka pembeni kabisa ya titi. kila titi lifanyia masaji kwa dakika kumi mara mbili kwa siku na matokeo huanza kuonekana angalau baada ya miezi mitatu.



tangawizi; hii ni njia ya asili sana ya kupunguza matiti hata kwenye jamii za zamani...tangawizi huongeza kasi ya mwili kuchoma mafuta pia na kupunguza mafuta yapatikanayo kwenye matiti.
jinsi ya kutumia;


chukua kijiko cha chai kilichojaa tangawizi ya unga kisha chemsha na kikombe kimoja cha chai kwa dakika kumi, kisha mimina kwenye kikombe na changanya na kijiko kimoja cha asali. kunywa vikombe viwili mpaka vitatu kwa siku.

green tea; haya ni majani ya chai ambayo yanapatikana sehemu mbalimbali nchini kwa sasa, majani haya yanaongeze kasi ya mwili kuchoma mafuta na hata kushambulia mafuta ya kwenye matiti.
jinsi ya kutumia;
weka majani ya chai kwenye kikombe chenye maji ya moto, funika kwa dakika tatu mpaka tano, ongeza kijiko cha asali.kunywa vikombe vitatu mpaka vinne siku.



mayai na limao; yai na limao pia ni bidhaa zinazotumika kupunguza ukubwa wa matiti na kufanya yawe magumu yaani kitaalamu kama tonicity, sasa chukua sehemu nyeupe ya yai na upake kwenye matiti na uache kwa dakika 30 kisha chukua limao changanya na maji na utumie mchanganyiko huo kusuuza matiti yako. fanya hivyo mara moja kwa siku.



virutubisho vya fish oil; vidonge hivi hutengenezwa kwa mafuta ya samaki, mafuta haya yana omega 3 ambayo kazi yake ni kuweka kiwango cha homoni za oestrogen mwilini katika kiwango sahihi, kama nilivyosema hapo mwanzo kiwango kikubwa cha homoni hii ni moja ya chanzo kikuu cha matiti makubwa.kidonge kimoja kwa siku kinatosha sana.[tuwasiliane ukihitaji suppliments hizi]
                            

acha kutumia njia za uzazi wa mpango za dawa; njia pekee ya uzazi wa mpango ambayo haitumii homoni ni kitanzi cha copper ambacho huwekwa kwennye kizazi hivyo ni salama, dawa zingine zote, sindano na vijiti zina homoni ambazo huchangia kuongezeka kwa ukubwa wa matiti.
mwisho; ni njia ya upasuaji tu yenye majibu ya haraka, njia hizi zingine zinahitaji nidhamu na uvumilivu kwani matokeo yake yanachukua muda mrefu.

SOURCE: SIRI ZA AFYA BORA

Post a Comment

11 Comments

  1. Boy mm ninamiaka 19 lk bdo yapo haya machuchu nifanyaje

    ReplyDelete
    Replies
    1. cha kufanya nikutumia hzo njia nilizoziorodhesha hapo juu..km utafata maelekezo vzuri utafaidika nazo..Jaribu hzo kwnza alafu baadae uje unipe matokeo yake

      Delete
  2. Mbñ matiti yangu hayakui?

    ReplyDelete
  3. Jmn mm nahitaji kupunguza matiti yananifanya nikose raha

    ReplyDelete
  4. Nahitaji izo supplements napataje

    ReplyDelete
  5. Dawa asili za kupunguza tumbo kitambi $$ kupunguza maziwa makubwa $$ kutengeneza shape ya mwanamke $$ matatizo ya uzazi ugumba. UTI sugu kuondoa uchafu na kunuka ukeni wasiliana na dr 0676039091 tanga

    ReplyDelete
  6. Dawa za kupunguza maziwa $$ kuongeza makalio& kutengeneza shape nzuri kwa wanawake $ kupunguza unene && kubana uke $$ wasiliana na dokta 0676039091 tanga

    ReplyDelete

Youtube Channel Image
Hajiizo Subscribe To watch more
Subscribe