Habari

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Advertise with us here

Burundi:Uchaguzi waahirishwa tena

Uchaguzi wa Burundi umeahirishwa tena.
Msemaji wa Rais Pierre Nkurunziza amesema uchaguzi utafanyika tarehe 21 Julai.
Uchaguzi huo umekumbwa na utata baada ya makundi ya upinzani kuandamana na kupinga hatua ya rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.

null

Upinzani unadai kuwa rais Nkurunziza anakiuka katiba ya taifa na mapatano ya Arusha yaliyokomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Kwa mujibu wa Msemaji wa rais ,Gervais Abayeho uchaguzi huo umeahirishwa kutoka tarehe 15 hadi tarehe 21 kufuatia shinikizo la viongozi wa kanda ya Afrika mashariki na Kati.
Viongozi hao wakiwemo mwenyekiti na mwenyeji wa jumuiya, rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, na Yoweri Museveni wa Uganda, rais wa Kenya Uhuru Kenyatta waliendekeza uchaguzi uahirishwe kufuatia mgogoro wa kisiasanchini Burundi.

 null
Shinikizo hilo la kuahirisha uchaguzi lilitokana na Umoja wa Afrika, na Umoja wa mataifa, jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki, pamoja na kikosi cha kimataifa kuhusu eneo la maziwa makuu.
Umoja wa Mataifa umesema kwamba idadi kubwa ya watu waliokimbia walisema nchi hiyo inakumbwa na msukosuko mkubwa wa kisiasa.

Zaidi ya raia laki moja wa Burundi wamekimbia nchi hiyo tangu mwezi Aprili wakati kulizuka ghasia kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Hii ilikuwa ni mara ya tatu kwa uchaguzi huo kuahirishwa baada ya tume ya uchaguzi kuahirisha uchaguzi kwa majuma matatu kutokea tarehe 26 Juni hadi tarehe 15 Julai

 Chanzo: http://www.bbc.com/swahili

Post a Comment

0 Comments

Youtube Channel Image
Hajiizo Subscribe To watch more
Subscribe