aijalishi kama maji ni machafu au maji ni masafi unacho hitaji ni kuyachuja na yatakua tayari kutumiwa.
Mfumo wa pikipiki hii unahusisha maji pamoja na betri ya gari, betri ya
gari inasaidia kutenganisha haidrojeni kutoka katika maji. Baada ya
kutenganishwa hydrogen hii hutumika kutengeneza nguvu inayoendesha
pikipiki hiyo.
Pikipiki hiyo inaweza kwenda umbali wa kilometa MIA TANO kwa kutumia LITA MOJA TUU ya maji!
Raia huyo wa brazil ambaye ni afisa jamii akielezea katika video hiyo
amesema kuwa moja ya faida ya kutumia maji ni kwamba haktakuwa na
uchafuzi wa mazingira maana shughuri hii hutoa mvuke na sio hewa ya
kaboni monoksaidi.
Katika video hiyo Azevedo anaonekana akinywa maji kuonesha kuwa kweli
ni maji kisha kuijaza katika pikipiki, baadaye anaonekana akichota maji
kutoka katika mto (uliochafuliwa) kisha anayajaza katika pikipiki na
kuondoka. Hii siyo mara ya kwanza kwa kutengenezwa pikipiki ikatumia
maji ila pengine hii inaweza kwenda mbali zaidi na kufikia hatua ya
kutengenezqa kibiashara.
0 Comments