Habari

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Advertise with us here

Unene wa kupindukia umekua ni moja ya matatizo yanayowasumbua wengi kiafya



Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na shirika la afya duniani, zaidi ya watu bilioni 1,5 duniani wamezidisha uzito wa miili yao na milioni 500 kati yao huwa na unene wa kupindukia au fetma.
Idadi hii ya watu wenye tatizo la unene wa kupindukia imeongezeka mara mbili tangu mwaka 1980.
Watu wengi wane tatizo hili huwa wanatokea katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea.
Tafiti zinaonyesha kuwa kila kipato kinapoongezeka ndivyo na kiwango cha tatizo la unene linavoongezeka.

Shirirka la afya dunini limetafsiri Fetma kama “mkusanyiko mkubwa wa mafuta ambayo hupelekea matatizo ya kiafya”.
Kila siku watu huhitaji kiwango fulani cha nishati kulingana na umri, jinsia, aina ya kazi wanazofanya, hali ya kimaumbile na kisaikolojia pamoja na hali ya kiafya.
Mafuta huchangia kati ya asilimia 15% hadi 18% ya uzito wa miili ya wanaume, wakati kwa wanawake mafuta huchangia kati ya asilimia 20 hadi 25% ya uzito wa miili yao.
Kama kutakua hakuna uwiano kati ya kiwango cha nishati inayoingia mwilini na kiwango cha nishati inayotumika, mafuta hujikusanya mwilini na hutokea tatizo la fetma au unene wa kupindukia.
Tatizo la fetma pia huathiri ubora wa maisha.Moja ya matatizo ambayo yanaweza kusababishwa na fetma ni kiwango kikubwa cha sukari katika damu, kisukari, presha, na magonjwa ya moyo.
Mengine ni kiwango kisicho cha kawaida cha mafuta katika damu, matatizo ya kibofu cha mkojo, athma au pumu na magonnjwa mengine ya mfumo wa upumuaji.
Kipimo ambacho hutumika kugundua tatizo la fetma ni BMI au kwa kirefu body mas index anbacho hulinganisha uzito na kimo cha mtu. Huchukuliwa uzito wa mtu katika kilogram na kugawanywa kwa kipeo cha pili cha kimo chake yaani Kg/m2.
BMI ya mtu mwenye urefu wa sentimita 180 na uzito wa kilogram 75 hupimwa kwa kuchukua 75 gawanya kwa 3.24 ambayo ni kipeo cha kimo cha mtu katika kipimo cha mita.
Jibu lake ambalo ni 23.15 linaonesha kuwa mtu huyu yupo katika kiwango cha kawaida. Kwa sababu wataalamu huchukulia kwamba ukiwa katika kipimo cha BMI kati ya 18.8 na 25 basi una uzito wa kawaida. Na kama majibu yako yataangukia baina ya 25 na 30 basi utakua una fetma.
Fasihi huigawanya fetma katika sehem tatu; watu wenye BMI kati ya 30 na 35 ambao huwa na uzito uliozidi, wenye BMI kati ya 35 na 40 ambayo huitwa unene wa kupindukia na wenye BMI zaidi ya 40 uzito usio kifani.

Lishe mbaya na isiyozingatia kanuni za afya pamoja na maisha ya kukaa kaa tu husababisha kiwango cha unene kuongezeka. Kula kiwango sahihi cha chakula na kufanya mazoezi kwa wingi ni nia nzuri ya kupambana na tatizo hili.
Baada ya kugundua namna tatizo hili lanavyoathiri watu wengi, shirika la afya duniani kwa kushirikiana na nchi kadhaa limeamua kuanzisha mafunzo kwa jamii ili kuwapa uelewa.
Wale ambao wanakaribia kufikia aina ya kwanza ya fetma wanaweza kuidhibiti kwa kufanya mazoezi kwa wingi.
Lakini vipi kuhusu wale wenye hali mbaya zaidi na unene wa kupindukia?? Je utaratibu maalum wa chakula pamoja na mazoezi yatawasaidia? Kwa bahati mbaya wataalamu hawana matumaini hayo kwa watu wa aina hii.
Wanasema kwamba kwa mtu ambaye kwa kawaida alitakiwa awe na uzito wa kilogram 75 lakini sasa ana uzito wa kilogram 150 au 200 huwa ni vigum kuirudia hali yake ya kawaida kwa kufuata taratibu za chakula na mazoezi tu.
Ushauri unaotolewa kwa watu wa aina hii ni operesheni hasa kwa watu wa aina ya tatu yaamni wenye uzito wa zaidi ya 40 katika kipimo cha BMI.
Tiba maarufu ambayo inafanywa siku hizi na wataalamu ni upasuaji ujulikanao kama “Bariatric surgery” ambao huwapa matumaini watu wenye matatizo haya.
Bariatric surgery ambayo huwa na hatua mbalimbali anazofanyiwa mgonjwa, huwa na lengo la kuongeza maisha ya mgonjwa kwa miaka 10 hadi 15.
Kwasababu matatizo yanayotokana na kuzidi kwa uzito yanaweza kuondoshwa kwa upasuaji tu na baadaye mazoezi hufuata. Wagonjwa wengi ambao hufanyiwa aina hii ya operesheni hupungua presha na kuondokewa na kisukari baada ya operesheni.
Hata hivyo madaktari wanasisitiza kuwa operesheni hii si ya urembo, bali hufanywa kwa mtu endapo anapata matatizo makubwa mno.
Wagonjwa huhitaji kupimwa na kuchunguzwa kwa makini kabala ya kufanyiwa tiba hii.
Kwa kuongezea madaktari wanapendekeza kuwa magonjwa yanayotokana na unene uliopindukia yatibiwe kwanza kabla ya operesheni kufanyika.
Madaktari wanasema kuwa kuna njia tatu za kufanya Batriatric Surgery ambazo ni kufunga tumbo, kuondoa sehemu ya nyama za tumbo na gastic by-pass.
Upasuaji huu hufanywa kwa njia ya kitaalamu ya kuingiza mirija myembamba na midogomidogo katika tumbo kupitia michanjo au chale ndogondogo. Wagonjwa hupunguza zaidi ya asilimia 70 ya uzito wao mwaka mmoja baada ya operesheni.

Uturuki ni moja ya nchi ambazo zinafanikiwa sana katika kufanya upasuaji huu wa Batriatric.
Wagonjwa wengi kutoka nje na ndani ya Uturuki hupendelea hospitali na vituo vya afya vya Uturuki kwa ajili ya tiba hiyo.

Post a Comment

0 Comments

Youtube Channel Image
Hajiizo Subscribe To watch more
Subscribe