Uvutaji wa sigara ni tabia ambayo imekua ikisababisha vifo
vingi vinavyozuilika…utafiti nchini marekani unaonyesha sigara imeua zaidi ya
mara kumi ya watu waliokufa kipindi cha vita zote ambazo marekani imepigana
kwenye historia yake..
Sigara huathiri mifumo yote ya mwili ya binadamu hasa mapafu
na kuua watu wengi katika umri mdogo sana. Kemikali iliyoko ndani yake maarufu
kama nikotini huharibu kabisa mifumo hii na kuucha mwili katika hali mbaya
sana.
Zifuatazo ni aina kumi za kansa za binadamu zinazosababishwa
na uvutaji wa sigara…
- Kansa ya mapafu; Hii ni aina ya kansa ambayo hushambulia mapafu, mgonjwa hukohoa sana na kutema damu.. huanza taratibu na haina matibabu ya kupona kabisa..mara nyingi huishia kwenye kifo..
- Kansa ya damu:Hii ni kansa ambayo hushambulia damu, mgonjwa huanza kwa kuvuja damu sehemu mbalimbali kama fidhi na puani, pia upungufu mkubwa wa damu mwilini.. na huua ndani ya mda mfupi sana kwa watoto na huchelewa kuua kwa watu wazima. Mwisho wa siku ni kifo tu.
- Kansa ya mlango wa uzazi:Kansa hii hushambulia mlango wa uzazi maarufu kama cervix, ikigunduliwa mapema huweza kutibiwa kwa mionzi na kupona kabisa.dalili zake ni kuvuja damu wakati wa tendo la ndoa, harufu kali sehemu za siri na maumivu makali ya tumbo la chini.
- Kansa ya figo:Hushambulia figo na kusambaa kwenye mishipa ya damu haraka sana..mara nyingi ni hugunduliwa kwenye steji za mwisho kabisa za ugonjwa..mgonjwa huanza kwa kukojoa damu na kuvimba mwili mzima.
- Kansa ya maini:Ni moja ya kansa ngumu sana kutibika.. watu wanaopata kansa hii huishi kwa mda mfupi sana. Na kufa ndani ya mwaka mmoja..dalili zake ni tumbo kujaa maji na kukonda sana..
- Kansa ya tumbo:Mgonjwa huanza kutapika damu na kukonda sana..matibabu yake ya kupona kabisa hayapo mara nyingi hua haina mwisho mzuri..
- Kansa ya utumbo mkubwa:Mgonjwa huanza na dalili za kutoa damu kwenye choo kubwa na kukonda sana.. hutibiwa kwa mionzi lakini mwisho wake sio mzuri..
- Kansa ya koo ya chakula:Mara nyingi mgonjwa hushindwa kutafuna chakula na kumeza, mwisho kabisa mgonjwa anawekewa mrija wa kupitishiwa chakula laini kama uji na mwisho unakua umekaribia.
- Kansa ya kongosho:Kansa hii huanza na maumivu makali ya tumbo, kupoteza hamu ya kula na kukonda.. hutibiwa kwa mionzi pia lakini mwisho wake sio mzuri..
- Kansa ya koo la hewa:mara nyingi mgonjwa hushindwa kuumua vizuri, kukohoa damu na kupungua uzito. Steji za mwisho koo la hewa huziba kabisa na mgonjwa hufa kwa kukosa hewa..
Mwisho: kuacha sigara mara moja na kukaa mbali na wavuta
sigara ndio mzizi mkuu wa kukwepa magonjwa haya..acha kujidanganya eti flani
ana miaka themanini mpaka leo hajafa na anavuta sigara. Ukweli ni kwamba kinga za
mwili za bidadamu hazifanani. Wewe ni wewe na yeye ni yeye..
0 Comments