Habari

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Advertise with us here

Hadi kufikia June 2013 hii ndio TOP 10 ya maajabu 10 ya Dubai

Miongoni mwa sehemu nzuri na zakuvutia kutembelea katika hii Dunia basi Dubai haiwezi kukosa, Dubai unatajwa kuwa mji wa kitalii na kibiashara, wengine wanautaja kama pepo ya watalii. Mji huo umejengeka kwa majengo yenye ramani za kuvutia. September 17 nakusogezea list ya maajabu 15 ya Dubai stori kutoka worldtoptop.com.

Hadi kufikia June 2013 hizi ni sehemu 10 zilizokuwa zinatajwa kuwa nzuri na zakuvutia Dubai.
  1. Burj al Arab

Burj_al_arab
Burj al Arab ni hoteli yenye hadhi ya nyota 7 ina vingi vya kuvutia, ikiwa ni pamoja na kuwa na uwanja wa tennis ulio juu, mgahawa chini ya bahari. Lakini Burj al Arab ni moja kati ya hoteli zinazoitambulisha Dubai.

2-Visiwa vya Palm

Jumeirah_palm_island_dubai
Visiwa vya Palm ni visiwa vikubwa zaidi vilivyotengenezwa na binadamu sio visiwa vya asili kama ilivyo kwa Zanzibar na vingine, visiwa hivyo vinatajwa kuwa miongoni mwa maajabu 8 ya Dunia.
3. Burj Khalifa

Burj-khalifa
Burj Khalifa inatajwa kuwa jengo refu Duniani lililojengwa na binadamu, Burj Khalifa ni jengo lenye ghorofa 160. 

4. Dubai Marina

dubai_marina
Dubai Marina ni mfereji mkubwa zaidi Duniani uliojengwa na binadamu, Dubai Marina una sehemu za kupaki boti ndogo lakini ni mji ambao umetengenezwa kuweza kuchukua watu 120000.

5. Infinity Tower

infinity_tower_dubai_2
Infinity Tower ni jengo refu lililojengwa katika mfumo wa nyuzi 90 na lina urefu wa futi 1000 kutoka chini.

6- Dubai Mall

dubai_mall_1 (1)
Dubai mall ni mall yenye eneo kubwa duniani na ina hifadhi ya wanyama ya kutengeneza, ina vyumba 250 vya Luxury hoteli lakini ina chem chem.

7. Jumeirah Beach Hotel

jumeirah_beach_wave_hotel
Jumeirah Beach Hoteli ni hoteli yenye hadhi ya nyota 5 , ramani yake ni kama wimbi la maji ya bahari.

8. Dubai Fountain

Dubai_fountain
Hii ni chem chem iliyopo Dubai kama hufahamu chemchem ni maji yatokayo ardhini lakini yanatoka yakiwa na presha.

9.  Atlantis The Palm Hotel & Resort

atlantis_hotel_dubai_1
Atlantis The Palm Hoteli & Resort ni hoteli yenye vyumba vya kulala chini ya maji ambapo ukilala katika hivyo vyumba unaweza pata nafasi ya kuona samaki wakubwa kama papa na wengineo.

10. Ski Dubai

Ski-dubai
Ski Dubai ni sehemu yenye theluji ina ukubwa wa mita za mraba 22500, inatumika kama sehemu ya kuenjoy kwa baadhi ya michezo ambayo huchezwa sehemu kama hizo.
 SOURCE >>> millardayo.com

Post a Comment

1 Comments

  1. its amazing....Dubai is a beutiful country compare to uerope countries

    ReplyDelete

Youtube Channel Image
Hajiizo Subscribe To watch more
Subscribe