MTAALAM wa program za kompyuta na mjasiriamali wa Marekani, Damir
Sabol, amevumbua program inayoitwa PhotoMath itakayotumika kwenye simu
za mkononi kukokotoa milinganyo ya hesabu na kutoa majibu hapohapo ndani
ya sekunde, vilevile program hiyo inafanya zaidi ya hayo aliyoyasema
Bw. Sabol.
"Mwanafunzi anaweza kuangalia swali kwenye kitabu chake na akaweza kukokotoa haraka na kupata majibu ya maswali ya hesabu kwa wepesi zaidi na kutambua kama amefanya vizuri (amepatia) au laa. Lakini cha zaidi ni kwamba mwanafunzi atapata fursa ya kuona hatua zote zilizopitiwa hadi kuweza kupata jibu sahihi kwa swali husika. Kwa hiyo si jambo la kupata jibu la swali tu, bali pia jinsi ya namna ambavyo swali hilo linafanywa pamoja na maelezo sahihi yenye kumfanya mwanafunzi aelewe kwa ufasaha jinsi jibu sahihi linavyopatikana.
PhotoMath ilianza kufanya kazi rasmi Oktoba mwaka jana jijini London na hadi sasa imepakuliwa katika mitandao zaidi ya mara million 11.
"Tulisikia kutoka kwa mama mmoja akisema, 'Sasa naweza kuwasaidia wanangu kukokotoa maswali ya hesabu’. Tukasikia pia kutoka kwa mwalimu mmoja akisema darasa lake lote kwa sasa linatumia PhotoMath," alisema Sabol.
Anaendelea kusema: “Kwa sasa tupo mbioni kutengeneza toleo jipya la program hii ambalo litakuwa na ufanisi mzuri zaidi wa lile la mwanzo kwani litaweza kufanya mambo makubwa zaidi ya hili ya kwanza na litakuwa na uwezo wa kukokotoa hesabu ngumu zaidi na kutoa majibu sahihi kwa muda mfupi sana.
"Katika toleo hili tutaanza na program inayofanya kazi kwenye teknolojia ya Android kwani ina soko kubwa kwa sasa na kwa kuwa ina watumiaji wengi zaidi, tunategemea mabadiliko makubwa zaidi na kuongeza watumiaji wa PhotoMath kwani tutaifanya pia iwe na mvuto mkubwa zaidi kwa watumiaji wake.”
Kampuni ya Sabol ya MicroBLINK, inajihusisha zaidi na kutengeneza program za kompyuta zinazotumika kwenye mifumo mbalimbali ya elimu duniani zikiwemo za malipo ya benki.
SOURCE: http://www.abdallahmagana.com
0 Comments