ugumba ni nini?
hii
ni hali ya wapenzi au mke na mume kutopata ujauzito baada ya kushiriki
ngono mbili kinga kwa muda wa mwaka mmoja mfululizo. ugumba unaweza kua
primary infertility yaani mtu hajawahi kubeba mimba kabisa tangu
azaliwe au secondary infertility yaani mtu ambaye amewahi kuzaa lakini
kwa sasa ameshindwa kubeba ujauzito. utafiti uanonyesha katika kila ndoa
tano au mahusiano matano ya kimapenzi basi uhusiano mmoja una matatizo
ya uzazi ya kushindwa kuzaa.
hali
hii imekua ikiongezeka kadri miaka inavyosonga mbele kwa sababu
mbalimbali kama mionzi ya mawasiliano yaani wi-fi , magonjwa mapya ya
binadamu na kadhalika. kwa wanawake utafiti mpya unasema uwezo wao wa
kubeba mimba unaanza kupungua baada ya miaka 30 ya umri kutokana na
kuanza kuishiwa nguvu kwa viungo vya uzazi. ugumba una vyanzo vingi sana
ambavyo vingine havifahamiki mpaka leo lakini hebu tuone vyanzo muhimu vya ugumba.
utoaji wa mimba;Huenda
hichi ndio kitakua chanzo kikuu cha ugumba miaka ijayo kwani siku hizi
kila karibia kila mwanamke ana sababu za kutoa mimba, utoaji wa mimba
una hatari nyingi ambazo huweza kuleta ugumba kama kuoza au kuharibika
kwa kizazi baada ya kushambuliwa na bakteria, makovu yanayoletwa na
vifaa vinavyotumika kutoa mimba kwenye mfuko wa uzazi na mlango wa uzazi
huweza kusababisha ugumba usiotibika.
matatizo ya vizaalishaji vya mayai [ovari];
ovari ni kiungo ambacho kinatoa yai moja kila mwezi ili liweze
kurutubishwa na mbegu ya mwanaume lakini kuna magonjwa ambayo yanaweza
kusababisha ovari hiyo ikaugua na kushindwa kutoa mayai, mwanamke ana ovari mbili lakini moja ikiuugua tu na nyingine haifanyi kazi mfano ugonjwa wa ovarian cyst.
matatizo ya mirija ya uzazi; ovari
zimeunganishwa kwenye mirija ambayo hupitisha mayai kwenda kwenye
mfuko wa uzazi..wakati mwingine mirija hiyo huziba kwa sababu mbalimbali
hivyo mayai hushindwa kupita na kusababisha ugumba.mfano ugonjwa wa endometriosis, upasuaji na peritonitis.
matatizo ya kizazi;
kizazi ndio sehemu kuu ambayo mtoto hutunzwa na kuishi kwa miezi yote
tisa, tatizo lolote linaloshambulia kizazi huleta ugumba. mfano, makovu
ndani ya kizazi, uvimbe ndani ya kizazi, kugeuka kwa kizazi na magonjwa
ya zinaa kama kaswende na kadhalika.
kansa; kansa ya
kizazi huzuia yai la mama lililorutubishwa kushindwa kujiweka kwenye
kizazi ili kukua, hivyo huchangia sana mimba kuharibika au kutotungwa
kabisa.
matatizo ya mlango wa uzazi; oparesheni
za kizazi, utoaji wa mimba na magonjwa ya zinaa huweza kusababisha
kuziba kwa mlango wa uzazi hivyo mbegu za kiume kushindwa kabisa kupita
kwenye mlango wa uzazi na kusababisha ugumba.
magonjwa mengine ya mwili; magonjwa yeyote ya binadamu ambayo huingilia mfumo wa homoni za uzazi huleta ugumba mfano magonjwa ya ini,kisukari, hyperthyrodism, na kadhalika.
matumizi ya sigara na pombe;
unywaji wa pombe sana na uvutaji wa bangi huzuia yai kutoka kwenye
ovari, lakini pia uvutaji wa sigara hupunguza uwezo wa yai kutembea
kutoka kwenye ovari kwenda kwenye mfuko wa uzazi na wakati mwingine
husababisha mimba kutunga nje ya kizazi.
msongo mkubwa wa mawazo;
ukiwa unatafuta mtoto tayari ukiwa umepaniki kwamba huenda usimpate
husababisha inasababisha mwili kutoa homoni kitaalamu kama cortisol
ambazo huzuia kazi za homoni za uzazi kitaalamu kama gonadotrophin
releasing hormone hivyo hali huzidi kua mbaya.
uzito uliopitiliza;
mwili mkubwa unaingilia mfumo wa utengenezaji homoni za uzazi hivyo
huweza kuleta ugumba katika umri mdogo sana, hivyo kupunguza uzito ni
moja ya njia bora kabisa ya kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kuzuia
ugumba.
mwisho;
kabla hujaanza kuzunguka kwa waganga wa kienyeji na mahospitalini ni
bora kujichunguza kama uko kwenye hatari zilizotajwa hapo juu. hakuna
dawa moja ambayo ina uwezo wa kutibu
ugumba kwa watu wote bila kutibu chanzo chake kwanza.... hivyo naweza
kusema kila mtu ana dawa yake ya ugumba kulingana na historia ya maisha
yake na chanzo cha tatizo lake. ugumba unaweza kupona kabisa kulingana
na chanzo cha tatizo na hali ya ugonjwa ilivyo na unaweza usipone kabisa
kama ugonjwa umeshapea sana, ndio maana kuna watu wenye uwezo mkubwa
sana wa kifedha, wasanii na wafanyabishara wakubwa lakini wameshindwa
kupata watoto pamoja na kwenda mpaka nje ya nchi na kuonana na madaktari
bingwa kwenye hospitali za kisasa kabisa.makala ijayo ntaongelea
matibabu ya ugumba kwa kina, usikae mbali.
SOURCE: DR. KALEGAMYE HINYUYE MLONDO >>> http://sirizaafyabora.blogspot.com
0 Comments