Hizi ni baadhi ya habari zilizoshika headlines leo katika baadhi ya magazeti ya Tz kama ulipitwa basi nimekuekea muhtasari mzima wa habari zilizoshika headline. Enjoy
MTANZANIA
MTANZANIA
Tume ya Taifa ya uchaguzi NEC,
imesema haina mpango wa kurudia uandikishaji wapigakura katika maeneo
waliyopita kwani inaamini kazi hiyo imefanywa kwa ufanisi wa hali ya
juu.
Pamoja na hali hiyo NEC imewaonya
wanasiasa kutoingilia kazi yao kwa sababu wanaifanya kwa mujibu wa
sharia za nchi, na hawapo kwa ajili ya kumwonea mtu bali kuandikisha na
kusimamia haki za wapigakura.
Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Waziri wan chi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenister Muhagama
kusema kuwa NEC itafanya uchunguzi kubaini kama kuna ameneo ambayo
wengi wameachwa bila kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapigakura
iliufanyike utaratibu wa kuandikisha.
Mwenyekiti wa NEC Damian Lubuva
alisema hata kama hali hiyo itajitokeza, watarfikiria namna ya kurudia
kazi hiyo, endapo utatolewa ushahidi wa wazi hasa kwa watu ambao
hawakupata bahati.
“Siku
ya mwisho kama kulikuwa na watu waliosalia ambao hawakuandikishwa
kwenye vituo ambao hawakuandikishwa na waliorodheshwa na wanajulikana,
tutafikiria, ikiwemo kurudia pale ambapo kutakuwa na ushahidi wa jambo
hilo” Lubuva.
Alisema si wajibu wa NEC kwenda kutafuta
watu eneo tofauti na lile lililopangwa kwa sababu hupangwa mapema mno
baada ya kutolewa matangazo.
MTANZANIA
Wauguzi wa Zahanati ya Serikali katika kijiji cha Shishuyi Wilaya ya Maswa, wanadaiwa kumfukuza mjamzito Rotha Bujiku
aliyefika katika Zahanati hiyo kwa ajili ya kujifungua na hatimaye
kujifungua kwa taabu katika bafu la mkazi mmoja kijijini hapo karibu na
Zahanati hiyo.
Watu walioshuhudia tukio hilo walisema
lilitokea majira ya saa 2 asubuhi wakato Rotha alipofika katika Zahanati
hiyo na kumkuta muuguzi Costansia John ambaye alikataa kumpokea.
Muuguzi huyo alikwisha kupewa maelekezo
tangu awali kuwa anatakiwa ajifungulie katika hospitali ya Wilaya ya
Maswa kwa kuwa amekuwa akizaa watoto mfululizo.
Wakati mama huyo akiendelea kulalamika
kutokana na uchungu aliokuwa akiupata, muuguzi huyo alimpigia simu
Muuguzi Mkunga wa zahanati hiyo na alipofika alimweleza mjamzito
kuondoka eneo hilo.
Rotha alilazimika kuondoa katika eneo hilo kusogea jirani na Zahanati hiyo na kujifungulia bafuni.
MWANANCHI
Boniface Mkwasa anakuwa
kocha ghali zaidi Mtanzania baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
kutangaza kumlipa Dola 12,500 (Sh28 milioni) kwa kukubali kuchukua
jukumu la kuinoa Taifa Stars.
Hiyo ni baada ya TFF kuamua kumpa kocha
huyo msaidizi wa Yanga, mahitaji yote pamoja na mshahara aliokuwa
akipokea kocha Mart Nooij, aliyetimuliwa Jumapili iliyopita baada ya
kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Uganda Cranes katika mchezo wa kusaka
kufuzu kwa Chan 2016.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi
alisema kuwa Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo imekubaliana kwa
pamoja kuwa Mkwasa apate stahiki sawa na zile za Nooij kama kielelezo
cha kuonyesha jinsi ambavyo utawala wake unavyothamini makocha wazawa.
“Nilikutana
na Mkwasa na kumwambia kuwa kile ambacho kocha aliyepita (Nooij)
alikuwa anapewa, tutahakikisha naye anapata, kuanzia gari, posho nyumba
na mshahara.
“Kwa
kuwa suala la mshahara na nyumba ni jukumu la Serikali, tayari
tumeshaiandikia barua kuwaambia kuwa tumeshapata kocha wa muda na
tunaomba apate mahitaji yote ambayo aliyemtangulia aliyapata,” Malinzi.
Malinzi pia amewashukia wachezaji wa
Taifa Stars pamoja na baadhi ya makocha kuwa wamechangia kwa namna moja
au nyingine kufanya vibaya kwa Stars kwenye michuano mbalimbali
inayoshiriki.
“Kama
Shirikisho tunapambana katika mazingira haya magumu tuliyonayo kwani
wachezaji wetu ni hawa hawa na hatuwezi kuchukua kutoka nje ya nchi.
“Sasa, watu wanamwangushia lawama Malinzi kama vile yeye ndiye anatakiwa kucheza wakati hiyo ni kazi yao wachezaji.
MWANANCHI
Mbunge wa Geita (CCM), Donald Max amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema kuwa mbunge huyo alifariki jana saa 12.00 jioni katika hospitali hiyo.
Ndugai alisema Max alikuwa mahututi kwa kipindi cha takribani miaka miwili iliyopita.
“Taratibu za maandalizi ya mazishi kwa sasa bado maana ni kama dakika 15 zilizopita ndiyo kafariki,” Ndugai.
Max alizaliwa Mei 22 mwaka 1957 na
kusoma katika Shule ya Msingi ya Salvatorian Convent na baadaye kujiunga
na Shule ya Sekondari ya Azania mwaka 1971 hadi mwaka 1974.
Mwaka 1980 alikwenda nchini Urusi na kusoma kozi ya ufundi katika Chuo cha Ufundi cha Roston on Don kabla ya kujiunga na Taasisi ya Volgograd Polytechnical nchini humo na kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika Uhandisi.
MWANANCHI
Polisi mjini hapa wameyasambaratisha maandamano ya watu wasiofahamika
waliokuwa na mabango ya kutaka muda wa uandikishwaji wa wapigakura
kuongezwa.
Watu hao, ambao polisi iliwaita ‘wahuni’, waliandamana saa tatu asubuhi kwenye Barabara ya Sokoine.
Haikuweza kufahamika mara moja watu hao walitoka wapi, kwani wenyeviti wa mitaa ya kata zote hawakuweza kuwatambua.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema walilazimika kutumia nguvu kuvunja maandamano hayo kwa vile hayakuwa halali.
Sabas alisema watu hao ni kundi la wahuni lililozuka kutaka kusitishwa uandikishaji wa wapigakura.
Diwani wa Kata ya Sombetini, Ally Bananga alisema hakuwa na taarifa na maandamano hayo, lakini hashangai kutokea kwake.
“Sitashangaa watu kuandamana,
kwani wamechoshwa na tabia ya watendaji kuwarudisha nyumbani. Watu
wanafika asubuhi kituoni wanaambiwa warudi nyumbani kwa sababu
hawakuandikisha majina yao,” alisema Bananga.
Mwenyekiti wa Mtaa wa JR, Jackson Mollel aliitaka tume kutoa mwongozo wa kuwasaidia wananchi kujiandikisha sehemu husika.
MWANANCHI
MWANANCHI
Mawaziri wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK)
na Wawakilishi kutoka CUF jana walitoka kwenye kikao cha bajeti cha
Baraza la Wawakilishi, wakipinga urasimu katika utoaji vitambulisho vya
ukazi wa Zanzibar na uandikishaji wapigakura.
Muda mfupi baada ya tukio hilo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
(SMZ) ilitoa taarifa yake ikisema kitendo cha mawaziri wa CUF kutoka
kwenye kikao cha bajeti ni kuvunja katiba, kwa kuwa wameshindwa
kuheshimu kiapo cha utii katika utekelezaji wa majukumu yao, kwa mujibu
wa Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1964.
Mawaziri hao walitoka nje ya kikao hicho muda mfupi baada ya Waziri
wa Miundombinu na Mawasiliano, Juma Duni Haji kusimama na kutoa
malalamiko ya kutoridhishwa na utendaji wa SUK katika kusajili na kutoa
vitambulisho hivyo vinavyotumika katika kuandikisha wananchi kwenye
Daftari la Wapigakura.
Wakati wawakilishi hao wanaondoka ndani ya ukumbi, wenzao wa CCM
walikuwa wakipiga makofi huku wakiimba “CCM, CCM, CCM”, na baadaye
baraza kuendelea na muswada wa kupitisha mapato na matumizi ya bajeti ya
mwaka 2015/2016.
Mawaziri waliohudhuria mkutano huo ni Abubakar Khamis Bakar ambaye ni Waziri wa Sheria na Katiba, Fatma Abdulhabib (Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais), Abdilahi Jihadi Hassan (Mifugo na Uvuvi) na Haji Mwadini Makame (Ardhi, Makazi, Maji na Nishati).
“Tumeamua kutoka ndani baada ya
kuona wenzetu tuliowaamini, wametubadilikia. Hawana nia njema ya
kuendesha serikali ya pamoja,” alisema makamu mwenyekiti wa CUF, Juma
Duni Haji alipoongea na waandishi baada ya kutoka kwenye ukumbi huo.
“Wameanzisha Serikali ndani ya Serikali na sasa wanawanyima haki wananchi kinyume na katiba.”
Duni alisema kwa miaka mingi wananchi wamekuwa wakizungushwa
kusajiliwa na kupewa vitambulisho vya ukazi, hali inayowaweka katika
hatari ya kupoteza haki zao za kijamii, ikiwa ni pamoja na fursa ya
kushiriki Uchaguzi Mkuu.
Hata hivyo, alisema uamuzi wao haujavunja katiba ya Zanzibar na kwa hiyo wataendelea na shughuli za Serikali kama kawaida.
Alidai kuwa kazi ya uandikishaji wapigakura kwenye Wilaya ya
Magharibi, Unguja imetawaliwa na vitisho na kwamba watu wasiojulikana
wamekuwa wakionekana wakiwa na silaha za moto na kujifunika vitambaa
usoni mithili ya maninja na wengine kuvaa vinyago.
NIPASHE
Serikali imesuuza roho za wastaafu nchini kwa kuwaongezea pensheni kutoka Sh. 50,000 wanayopata sasa hadi Sh. 100,000 kwa mwezi.
Serikali imesuuza roho za wastaafu nchini kwa kuwaongezea pensheni kutoka Sh. 50,000 wanayopata sasa hadi Sh. 100,000 kwa mwezi.
Hata hivyo, serikali imekataa kuondoa tozo la Sh. 100 kwa kila lita
ya mafuta fedha zitakazoelekezwa katika miradi ya umeme vijijini (REA) na miradi ya maji vijijini.
Katika Bajeti iliyosomwa Juni 11, mwaka huu, serikali ilipendekeza
nyongeza ya pensheni kutoka Sh. 50,000 hadi Sh. 85,000 kwa mwezi.
Aidha, tozo ya mafuta ya dizeli na petroli kutoka Sh. 50 hadi 100
kwa lita na mafuta ya taa kutoka Sh. 50 hadi 150 kwa lita ili kuondoa
uchakachuaji.
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, akijibu hoja
mbalimbali za wabunge jana alisema jumla ya wabunge 98 walichangia
mjadala moja kwa moja na wengine 13 kwa maandishi.
Alisema kwa kushirikiana na Kamati ya Bajeti, wametafakari michango
ya wabunge 17 na kuona kiasi cha pensheni kilichoongezwa na serikali,
bado hakitoshi na kwa kuzingatia kuwa ni wazee walioshiriki jitihada za
kuleta maendeleo na kulifikisha taifa hapa lilipo.
“Kuanzia Julai Mosi, mwaka
huu, wastaafu wa kima cha chini watatoka Sh. 50,000 hadi Sh.
100,000…tutaimarisha mifumo yetu kuhakikisha wanaopunjwa, wanaokosa
fedha zao, wananyanyaswa na watendaji, inakuwa thabiti pale alipo
anapata pensheni yake.“
Waziri huyo alisema wapo watendaji ambao wanashindwa kutoa majibu
sahihi kwa wazee wanaofika Hazina na wanachukuliwa hatua na wataendelea
kuchukuliwa kwa kuwa ni haki ya wazee na siyo upendeleo kwa kuwa
wamechangia maendeleo ya taifa.
Alisema hoja ya mafao ya uzeeni ilichangiwa na wabunge 14, serikali
imejipanga kuwatambua wazee kote nchini kwani kwa mujibu wa Takwimu za
Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, wapo milioni 1.2 na kwa sasa kuna
ongezeko zaidi hadi mwaka huu kwani kuna waliofikisha umri na wengine
wamefariki dunia.
“Kwa idadi hiyo tukisema
tulipe kila mmoja Sh. 10,000 kila mwezi, tutahitaji zaidi ya Sh. bilioni
140, lakini hatujui makazi yao yalipo, hivyo kwa mwaka 2015/16, tunatoa
fedha kwa maofisa wetu waende kuwatambua mahali walipo, tuwawekee mfumo
ambao watapata fedha zao walipo,” alifafanua.
Alisema siyo wazee wote waliokuwa serikalini, lakini walichangia
Pato la Taifa kwa shughuli zao kwenye sekta mbalimbali na kilio chao
kimesikika na yote ni utekelezaji wa sera ya mafao kwa wastaafu.
Mkuya alisema serikali inafanya hivyo kwa kuwa kuna ripoti ya
pensheni zinazopelekwa, lakini wahusika hawapati kutokana na mifumo na
maofisa ambao siyo waaminifu wamekuwa wakishirikiana na benki kuchukua
fedha hizo.
NIPASHE
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk.Harrison Mwakyembe
amesema kufungiwa kwa Tanzania kuuza mcheze katika soko la Afrika
Mashariki linashughulikiwa na litapitiwa ufumbuzi ndani ya miezi miwili.
Kauli ya Mwakyembe imekuja siku chache
baada ya Baraza la mchele Tanzania RCT kuiomba Serikali kushughulikia
kufunguliwa kwa wafanyabiashara wa Tanzania wauze mchele katika soko la
EA.
Mwakyembe alisema uamuzi wa kufungiwa kwa Tanzania naufahamu na jambo hilo linashughulikiwa.
Alisema hatua alizoanza kuchukua ni pamoja na kukutana na Waziri wa viwanda na biashara wa Rwanda kujadili suala hilo.
“Tatizo
lilikuwa kwa baadhi ya wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu waliokuwa
wakiingiza mchele kutoka nje na kuuchanganya na mchele wa ndani kasha
kasha kuuza katika soko la Afrika Mashariki,”Mwakyembe.
Alisema nchi wanachama wa EA wana sharia
ya kusameheana ushuru wa bidhaa zinazozalishwa katika nchi hizo pamoja
na kodi ndogondogo.
HABARILEO
Serikali imekubaliana na umoja wa
madereva katika madai yao waliyokuwa wakihitaji yatekelezwe, hali ambayo
imemaliza tishio la kuwepo mgomo kwa mabasi yanayoenda mikoani pamoja
na yale yanayofanya safari mijini.
Madai hayo ni pamoja na kupewa mikataba ya kudumu na waajiri wao, kukatiwa bima za afya pamoja kuongezewa mishahara.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa
kikao kilichofikia makubaliano hayo, Katibu wa Umoja wa Madereva
Nchini, Rashid Said alisema Serikali imekubali kusimamia na kutekeleza
madai ya madereva ili kuepusha migomo ya mara kwa mara na kusababisha
adha ya usafiri.
“Tumemaliza
kikao chetu na mambo yote tuliyokuwa tunahitaji yatekelezwe
yamekubalika. Lakini tumewaambia yatekelezwe ndani ya siku chache hizi
na ifikapo Julai mosi mwaka huu kama hayajatekelezwa mgomo utakuwa pale
pale,” Said.
Alisema wamefurahishwa na maamuzi ya
kikao hicho ambayo yatakuwa ni mkombozi wa maisha ya madereva, kwani kwa
muda mrefu wamekuwa hawanufaiki na kazi yao zaidi ya kuwazalishia
wamiliki kiasi kikubwa cha utajiri, lakini wao kubaki katika hali duni
ya maisha.
Hivi karibuni madereva walitishia
kuanzisha mgomo endapo Serikali haitayashughulikia madai yao ambayo kwa
muda mrefu wamekuwa wakipiga kelele yatekelezwe.
Mgomo wa madereva nchini ulitokea
mwanzoni mwa Mei mwaka huu na kudumu kwa siku mbili na kusababisha kero
mbalimbali kwa wasafiri huku asilimia kubwa ya wananchi wakitembea
wakati wakienda katika shughuli zao mbalimbali huku waliokuwa wakienda
mikoani kukwama katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo.
Hata hivyo, mgomo huo ulisitishwa baada
ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuunda Tume ya kushughulikia madai ya
madereva ambayo hadi jana ilikuwa ikiendelea kujadiliana.
0 Comments