Katika hali ya ghafla Serikali ya India imetoa agizo la kuzuia mitandao inayoeneza picha, video n.k za ngono kupatikana nchini India. Mara moja watoa huduma wa intaneti mbalimbali wameanza kufuata agizo hilo. Uamuzi huo ambao ukaanza kulaaniwa na wengi mara moja umekuja baada ya maombi ya watu kadhaa kuwepo mahakani tayari kwa muda mrefu ya kupinga upatikanaji wa mitandao ya mambo ya ngono nchini India.
Kupitia mitandao ya kijamii tayari
watu wengi nchini humo wameungana katika kupinga uamuzi huo wa serikali ya
India kuzuia (ban) zaidi ya mitandao 850 ya kingono ikiwepo maarufu zaidi kama
vile PornHub, YouPorn na mingine mingi.
Wengi wanasema uamuzi huo unaingilia uamuzi wa
mtu binafsi huku wakidai hawaoni jinsi mtu anavyovunja sheria au kufanya makosa
pale anapokuwa chumbani/nyumbani kwake na kuangalia picha hizo. Wanadai uamuzi
huo wa serikali unaingilia haki ya uhuru binafsi wa wananchi ambao unalindwa
kikatiba.
Tayari baadhi ya watoa huduma za
internet washaanza kufuata agizo la serikali lakini bado wengine wamekataa
wakisema watakuwa wanavunja haki za wateja wao. Watafiti mbalimbali wanasema
uamuzi wa serikali ata ukifuatwa hautaweza kuwa na nguvu sana kwani watu
wanaweza jifunza kutumia teknolojia za maficho kama vile ya VPN ambazo
zitawawezesha kutembelea mitandao hiyo bila tatizo huku watoa huduma za
intaneti na serikali kutokuwafahamu kabisa.
Wanaounga mkono maamuzi hayo wanadai
uwepo wa mitandao hiyo unachangia katika uwepo na ukuaji wa makosa ya kingono
kama vile ubakaji.
Je, kwa mtazamo wako unadhani sheria kama hii ingeletwa Tanzania ingepunguza ongezeko la vitendo vya ubakaji na uasharati?
0 Comments