Habari

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Advertise with us here

BONDIA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA Knockout? - South Afrika

boxing_ring_1 
Stori kutoka South Africa inahusu taarifa ya majonzi ambapo Bondia mmoja, Mzwanele Kompolo ambaye alipanda Ulingoni kwenye Pambano la ufunguzi siku ya Jumanne September 15 2015 alifariki muda mfupi baada ya kupigwa kwa knockout kwenye Round ya kwanza kabisa kwenye pambano lake na Bondia mwingine,  Siphenathi Qampi.

Marehemu Mzwanele alianguka na kupoteza fahamu akiwa kwenye Pambano hilo, baada ya jitihada za madaktari wa uwanjani hapo kuonesha hakukuwa na dalili za hali yake kuwa sawa, ilibidi apelekwe Hospitali ambapo fahamu zake hazikurudi mpaka baadaye alipofariki.

Matukio ya Mabondia kufariki Ulingoni sio mageni Duniani, Phindile Mwelase alikuwa Bondia wa kike ambaye na yeye alifariki October 2014 South Africa baada ya damu kuvujia kwenye ubongo akiwa kwenye pambano, mwingine ni David Browne Jr ambaye alifariki Australia jumanne September 14 2015 baada ya kupigwa kwa Knockout pia kwenye pambano Australia.

Hiki hapa kipisi cha Video kifupi kilichorekodiwa dakika za mwisho za Bondia Mzwanele Kompolo uwanjani.

SOURCE: millardayo

Post a Comment

0 Comments

Youtube Channel Image
Hajiizo Subscribe To watch more
Subscribe