#EastAfrika
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza kwamba June 2016 mradi wa ujenzi wa barabara za Treni za kisasa za kusafirisha watu kwenye jiji la Nairobi utazinduliwa rasmi.
Taarifa niliyoidaka kupitia mtandao wa Nation ni kwamba serikali ya Kenya inashirikiana na nchi ya Hungary kwenye ujenzi wa mradi huu ambao utafanana na ule wa Addis Ababa Ethiopia ulioanza kufanya kazi September 2015.
Miradi ya Treni kama hizi maarufu kwa jina la Tram
ipo kwenye nchi zilizoendelea kama Hispania ambapo President Uhuru
amesema shilingi bilioni 15 za Kenya zinatengwa kwa ajili ya hii
shughuli ya kuondoa foleni kwenye jiji la Nairobi, jiji linalotajwa kuwa
la kwanza kwa foleni Afrika Mashariki likifatiwa na Dar es salaam.
Barabara zitakazo husika kwenye mradi huu ni pamoja na Thika Superhighway, Ngong Road, Limuru Road na Ongata Rongai ambapo
balozi wa Hungary Kenya amesema Treni hizo zitakua na uwezo wa
kusafirisha abiria zaidi ya laki tatu kwa siku na itakua zaidi ya hiyo
idadi iwapo matawi yote yatakamilika.
Taarifa niliyoidaka kupitia mtandao wa Nation ni kwamba serikali ya Kenya inashirikiana na nchi ya Hungary kwenye ujenzi wa mradi huu ambao utafanana na ule wa Addis Ababa Ethiopia ulioanza kufanya kazi September 2015.
Kwa ndani..
Treni ya Addis Ababa Ethiopia ilivyokua ikizinduliwa.
Ujenzi wa barabara ya Treni Ethiopia.
0 Comments