Unakumbuka ulipotumia njia nyingi kumpata mpaka akawa chini ya himaya yako? Unakumbuka jinsi ilivyomuwia vigumu kukuamini na kukupa moyo na mwili wake? Sasa Mbona umemgeuka kirahisi hivyo. Brother hauna huruma hata punje.
Sasa usikasirike pale atakapopata moyo wa kusonga mbele na kukuacha kama hamjawahi ku date vile. Usianze kumsumbua na kumwambia kuwa umemkumbuka. Utakua umechelewa sana.
Mpende hivi sasa, appreciate mapenzi yake kwako hivi sasa wakati bado yupo. Usimuumize, usimuoneshe dharau ya wazi..anumia, moyo unauma..mapenzi yanaumiza. Usimlize tafadhali. Akiondoka itahitaji maajabu kurejea.
Wanawake waaminifu ni wazuri sana, ila inahuzunisha sana kwani wao ndio wanaongoza kwa kuumizwa. Uaminifu wao unawaponza.
#LiveLove
0 Comments