Nina miaka 32, mimi na mume wangu tulikuwa ktk uhusiano kwa miaka 6. Tulikuwa marafiki kweli kweli. Nilimsubiri mpaka amalize chuo na aanze kazi.
Familia yangu na familia yake zilikutana, tulioana na tunamtoto mmoja (miaka 7 sasa)
Mume wangu alikuwa ni mtu mwenye hasira, ila tatizo lilianza pale nilipoanza kumuonesha kwamba hawezi kunitawala mimi. Kila muda tulipokwaruzana, nilipaki vitu vyangu na kwenda kwetu kuwaelezea matatizo ya mume wangu.
Dada zangu wangempigia simu na kumkaripia. Kila tulipokwaruzana ambapo mara nyingi chanzo nilikuwa mimi mwenyewe nilimweleza kama anahitaji anipe talaka tu me sina shida na hiyo ndoa
Ila kiuhalisia sikuhitaji talaka.
Nilikua na majivuno na kiburi na sikuhitaji nionekane kama mwanamke aliye looser machoni pake.
Kuna siku moja nilimuudhi, tulikwaruzana hivyo nikamsukuma akaanguka na hii ilikuwa mara ya kwanza kwa yeye kunipiga, kuniumiza, kunitoa nje na kufunga mlango.
Nilienda kwetu na familia yangu ilinichukua na kunipeleka polisi ktk dawati la jinsia kwa kuwa nilijionesha kuwa nanyanyaswa na mume wangu. Ila kiukweli mimi ndio nlikua namnyanyasa mume wangu.
Alikamatwa na polisi na kusekwa rumande, niliombwa na familia ya mume wangu kufuta kesi ila wala sikukubaliana nao.
Moyoni nilitambua kuwa nilichofanya sio sahihi kwa sababu mume wangu sio mpigaji, alifanya vile kwa sababu nilimsukuma ukutani hvyo akapandwa na hasira na kunipiga.
Nilifuta mashtaka na tukayamaliza kifamilia.
Baada ya miezi mitatu, nilibeba mabegi yangu na kuondoka hii ni kutokana na kukwaruzana kidogo tu. Hivyo alibaki peke yake. Baada ya siku mbili nikapokea simu kwamba anaumwa amelazwa hospitali.
Familia yangu ikanikataza na kuniambia kwamba nikienda nitaonekana nabembeleza ndoa na dada zangu wakanihakikishia kuwa atakuwa anajifanyisha kuumwa ili mimi niende.
Muda wote huo ndugu zangu walikuwa wakinionea huruma wakidhanj mimi ndio nanyanyaswa na mume wangu.
Alikaa wiki moja hospitalini, akatoka na kuanzia siku hiyo nikapewa taarifa ya talaka rasmi. Kiuhalisia sikuhitaji talaka. Nilitaka nikatae lakini kwa kuwa nilikuwa na majivuno nlitaka yeye ndio abadilishe mawazo na kinibembeleza.
Tulipoenda mahakamani kushughurikia talaka, nilitaka kumkomoa kwa kumfanya alipe, hivyo niliiambia mahakama imuamuru kugawana mali zote nusu kwa nusu.
Kwa mshangao wangu kwa moyo mweupe kabisa akaiambia mahakama mali zote ambazo mimi na yeye kwa pamoja tumezitafuta nipewe mimi. Yeye anachohitaji ni talaka tu.
Tulipeana talaka hiyo ilikuwa mwaka 2010.
Leo hii naandika waraka huu mume wangu anaoa mke mwingine, wakati mimi nipo tu kwa wazazi wangu, mali zote walinishauri niuze! Ndugu zangu kazi yao kila siku ni kuniteta.
Nategemea kile ambacho mume wangu wa zamani anakitoa kwa ajili ya mtoto nami ndio ntumie hicho kwa ajili ya kuishi.
Najua nlipoteza ndoa yangu kwa uzembe wangu mwenyewe.
Nipo hapa kuwaambia wanawake wote kwamba kuweni makini na ushauri mnaopewa unaolenga ndoa na mahusiano yenu.
Usidanganyike, usiruhusu familia yako iingilie ndoa yako, akili za kuambiwa changanya na zako.
Hivi sasa hata wadogo zangu wanaheshimiwa zaidi kuliko mimi. Wale walionisisitizia kudai talaka ndio wanaonisema vibaya hivi sasa.
Tafadhali sana wanawake kuweni makini na mahusiano yenu. Niliona ni vema ku share story yangu hii kuoakoa ndoa zenu.
There is no benefit in pride. Think about it!
0 Comments