kuna mambo kadhaa ya msingi sana ambayo usipokua makini nayo utampoteza mtoto kama ifuatavyo:-
hakikisha anapata chanjo zote; ukiona unaambiwa mtoto anatakiwa achomwe chanjo fulani maana yake ugonjwa unaozuiliwa na chanjo hiyo umeshaua watoto wengi sana hivyo ukileta uzembe tu mtoto wako anaweza kua mmoja wa watakao uwawa na ugonjwa huo.
mpeleke hospitali akiugua; mara nyingi akina mama hunza kutibu wenyewe na wakiona mtoto amezidiwa kabisa ndio wanakimbia hospitali, mara nyingi watoto hawa wanapona kwa bahati tu lakini wengi hufariki..mtoto sio kama mtu mzima akiugua kidogo tu anafariki hivyo usilete uzembe katika hili.
tumia neti ya mbu; kama wewe neti huiwezi basi nunua kitanda maalumu cha mtoto usiku akilala alale na net, malaria inaongoza kwa kuua watu hapa afrika na watoto wakiuawa zaidi kuliko hata watu wazima.
kula vizuri mlo kamili; ili upate maziwa ya kutosha yenye virutubisho vyote hakikisha unakula vizuri kwa kufuata mlo kamili yaani mchanganyiko wa vyakula vyote, kipindi mtoto ananyonya achana na mawazo ya kupungua uzito, subiri afikishe miaka miwili ya kunyonya ndio uanze kupungua lakini pia mifupa, nyama na kila kitu cha mtoto kinatokana na wewe hivyo kula vizuri kurudishia madini yaliyopotea wakati wa ujauzito...usipozingatia hili utakutana na upungufu wa madini siku za usoni
osha matiti yako kila ukitaka kunyonyesha; akina mama wengi wana shughuli nyingi hatukatai lakini tabia ya kunyonyesha bila kuosha matiti wakati wa shughuli hizo ndio chanzo cha mtoto kuharisha mara kwa mara. ukitoka kwenye shughuli zako oga au osha matiti afu ndio umpe mtoto anyonye.
fuata ushauri wa daktari; usipende kutoa dawa hovyo bila kupata ushauri wa daktari au muhudumu wa afya, dawa hizo hutolewa kwa uzito na mara nyingi uzito wa mtoto huongezeka kila mara hivyo dozi aliyopewa miezi mitatu iliyopita huenda mwezi huu haimtoshi tena.
achana na maziwa mbadala; kama hauna jinsi labda wewe ni muathirika wa ukimwi na umekatazwa kunyonyesha au hauna maziwa ya kutosha basi unaweza kumpa mtoto maziwa ya ngombe au maziwa ya dukani lakini nikuthibitishie kwamba maziwa ya mama hayana mbadala wa 100%, yale ya mama ni bora zaidi kwa afya ya mwili na akili za darasani hapo baadae.
weka hatari zote mbali na mtoto; mtoto asipelekwe jikoni kwenye moto, usiweke dawa zozote mahali pa wazi yaani dawa za panya, dawa za binadamu na kadhalika, nyumba yako hakikisha haina shimo hata moja na hakikisha mtoto hachezi barabarani yaani hatari zote weka mbali.
simamia maendeleo ya mtoto; baadhi ya wanawake wako bize sana na maisha baada ya kujifungua hivyo kazi ya kulea huwaachia wafanyakazi wa ndani, ni hatari sana kukabidhi maisha ya mtoto wako kwa mfanyakazi..jitahidi uende clinic hata mara moja moja ujue maendeleo yakoje, jifunze jinsi ya kusoma kadi ya clinic kujua kama uzito unapanda au unashuka, rudi nyumbani ghafla ukague kama mtoto anapewa chakula kama unavyotaka.
kua makini usibebe mimba mpya kabla huyo mdogo hajakua; kunyonyesha tu kunaweza kuzuia mimba lakini kama mama ananyoshesha zaidi ya mara kumi kwa siku ndani ya miezi sita ya kwanza kama huwezi kutumia kalenda au damu hazijaanza kutoka basi chagua njia ya uzazi wa mpango ambayo ni salama kwa mtoto.
Source: SIRI ZA AFYA BORA
0 Comments