Habari

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Advertise with us here

NAFASI ZA MASOMO MAURITIUS

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI INATANGAZA
NAFASI ZA MASOMO ZILIZOTOLEWA NA SERIKALI YA
MAURITIUS, NGAZI YA SHAHADA YA KWANZA KWA MWAKA WA
MASOMO 2017-18

 Image result for wizara ya elimu zanzibar
 
1 Sifa za muombaji
  •  Asiyezidi miaka 25
  • Awe amemaliza kidato cha sita na amefaulu daraja la kwanza au la pili au amehitimu ngazi ya Diploma.
2 Utaratibu wa malipo
Waombaji watakao bahatika kupata nafasi hizo watapatiwa malipo
yafuatayo;
  1. Posho la kila mwezi Rs 8,300 kwa USD 266
  2. Ada ya masomo Rs 100,000 kwa USD 3205 kwa mwaka
  3. Tiketi kwa kipindi chote cha masomo hadi kumaliza.
3 Njia za kufanya maombi
Waombaji wote wanatakiwa waombe barua ya kujiunga na chuo
(Admission Letter) kupitia mitandao ya vyuo vya Mauritius kama
vifuatavyo;
CHUO na ANUANI
  1. University of Mauritius www.uom.ac.mu
  2. University of Technology, Mauritius www.utm.ac.mu
  3. Universities des Mascareignes www.udm.ac.mu
  4. Fashion & Design Institute www.fdi.ac.mu
  5. Mauritius Institute of Education www.mie.ac.mu
  6. Mahatma Gandhi Institute www.mgirti.ac.mu
  7. Rabindranath Tagore Institute www.mgirti.ac.mu
Fomu ya maombi na maelekezo yake inapatikana katika mtandao
ufuatao;
http://ministry-education.govmu.org/English/Scholarships/
Pages/default.aspx
4. Utaratibu wa kuwasilisha maombi
Waombaji wa nafasi hizo watatakiwa kuwasilisha viambatisho vifuatavyo
katika maombi yao;
  1. Cheti cha kuzaliwa
  2. Vivuli vya Vyeti vya kumalizia masomo vya “O” na “A” Level
  3. Fomu ya Afya (Medical Report)
  4. Kivuli cha pasi ya kusafiria
  5. Nyaraka zote zinahusiana na masomo anayotaka kusomea
Kwa maelezo zaidi Kuhusiana na nafasi hizo fika;
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali – Kitengo cha
Uratibu wa Elimu ya Juu chumba No.57.

Post a Comment

0 Comments

Youtube Channel Image
Hajiizo Subscribe To watch more
Subscribe