Kuna msemo unasema kwamba kila mtu
ni muongo hapa duniani yaani , hakuna mtu ambaye ameshawahi kuishi bila kusema
uongo kabisa..
kitaalamu mtu akiulizwa swali
akajibu uongo, hali ya mwili hubadilika yaani mapigo ya moyo hukimbia, presha
hupanda na anaweza hata kutokwa jasho.
kipimo cha polygraphy hutumia njia
hii kufahamu kama mtu anadanganya au vipi kwa kuangalia mabadiliko ya mfumo wa
mwili pale anapokua anaulizwa maswali, mara nyingi kipimo cha polygraphy
hutumika na askari polisi kwenye nchi zilizoendelea kuwagundua wahalifu lakini
pia baadhi ya vipindi vya mahusiano kwenye tv huweza kuwapima wapenzi au
wanandoa kujua kama mmoja wao sio muaminifu.
sasa katika njia za kijasusi,
inawezekana kujua mtu, rafiki yako, ndugu yako, mpenzi wako au mke wako
anakudanganya kwa kuangalia vitu muhimu wakati wa kumohoji muhusika bila kua na
mashine na kujua kwamba anakudanganya kama ifuatavyo.
kuchelewa kujibu swali; ukimuuliza mtu swali akachelewa kujibu kuna uwezekano
mkubwa anadanganya lakini inategemea na aina ya swali ulilolo muuliza, kwa
mfano ukimuuliza sikukuu ya christmas mwaka 2005 ulikua wapi? kwa hali ya
kawaida lazima atafikiria kabla ya kutoa jibu na hatatoa jibu la uhakika sana
lakini ukimuuliza miaka mitano iliyopita ulinisaliti na mwanaume mwingine kama
hakukusali atajibu haraka kwa mshangao kwamba sio kweli lakini kama ni kweli
alikusaliti akili yake itaanza kuwaza huyu mtu kajuaje na atachelewa kujibu
kisha baada ya muda atatoa jibu la kukana au atadanganya.
kukosekana mahusiano ya maneno na
vitendo; kwa hali ya kawaida mtu akiulizwa
swali na akatakiwa kujibu ndio au hapana kama ni ndio atatikisa kichwa kwenda
juu na kama sio kweli atatikisa kichwa kwa pembeni sasa mtu akiulizwa swali
akadanganya ataenda tofauti na hali ya kawaida mfano ukimuuliza kwamba ulienda
kazini? atajibu ndio huku anatikisa kichwa kwenda pembeni bila yeye kutambua
kwamba ulimi wake ndio unakubali lakini mwili wake umekataa.
kukohoa kidogo au kumeza kabla ya
kujibu; mtu akipata wasiwasi baada ya
kuulizwa kitu ambacho kimemkosesha amani kitaalamu mfumo wa mishipa ya fahamu
kama sympathetic pathway unakua umefanya kazi hivyo mate yatakauka mdomoni na
kwenye koo hivyo kuondoa hiyo hali atakohoa kidogo au kumeza mate kabla
hajajibu ili kupata muda zaidi wa kutafuta cha kudanganya.
kuficha macho au mdomo kwa kutumia
mikono; hii hutokea bila yeye kufahamu
kitaalamu kama subconcious level yaani kibinadamu anashindwa kuuvumilia ule
uongo anaosema hivyo atajikuta mwenyewe anaweka mikono sehemu hizo bila kujua
ila wewe unayemuuliza maswali ndio utagundua kwamba anadanganya.
kushika shika sana sehemu za kichwa
chake; kama nilivyosema hapo juu, mfumo wa
sympathetic system ukianza kufanya kazi mishipa ya damu huanza kujikunja hasa
na sehemu zinazokosa damu hasa usoni huanza kuwasha kwa mbali na kua tofauti
hivyo muongo atajikuta anakuna pua, anakuna sikio na hata viganja vya mikono.
kuhangaika mazingira yanayomzunguka; mtu anayedanganya akiulizwa swali anaweza kuanza kuanza
kurekebisha vitu ambavyo viko sahihi kwa mfano kurekebisha tai,miwani,
kuchomekea vizuri...kama ni mwanamke muongo ataanza kuweka nywele vizuri na
kurekebisha sketi yake kabla ya kujibu kumbuka kama akifanya vitu hivyo baada
ya kujibu sio muongo au unamuuliza mtu swali amekaa mezani ghafla kila kitu
kimebadilika sehemu kilipokuwepo yaani kahamisha glass ya maji, funguo zake,
simu na kadhalika.
kushindwa kukuangalia usoni; unaweza ukaanza kumuuliza vitu vya kweli kabisa huku
mnaangaliana lakini ghafla chomeka swali la tofauti ambalo unataka kujua kama
ni kweli au sio kweli basi utaona anaanza kungalia pembeni na kushidwa
kuangalia usoni na wakati mwingine kijasho chembamba kitamtoka.
kua na maneno mengi sana; unaweza ukampigia simu ukamuuliza mtu kwamba yuko wapi
akakujibu nilienda hospitali kuona mgonjwa njiani kidogo ningatwe na mbwa afu
nimechoka sana ntajitahidi leo nilale mapema na kadhalika...huyu anaweza kua
medanganya kitu sasa anajaribu kukificha na maneno mengi ili usimjue lakini
ukute kwa hali ya kawaida angesema niko hospitali kisha akakaa kimya.
kupunguza sauti; mtu kama huyu unaweza kaunza kumuuliza mambo anayofahamu kwa
uhakika mfano jina lake, miaka yake, anaishi wapi au kama ni mchumba wako
unaweza kumuuliza rafiki yake anaitwa nani, anafanya kazi gani na hapo atakua
mchangamfu na kujibu vizuri kisha ghafla ukamuuliza nasikia umelala na mwanaume
fulani hapo sauti itakua ndogo na atakataa kwa sauti ya chini.
kuapa mara nyingi; mtu muongo hujitahidi sana kujitetea aonekane hana kosa
yaani kila baada ya muda ata apa kwa mungu, atakua na kauli kama 'ukweli kutoka
moyoni", atasema hichi nachokisema hapa ni kweli kabisa lakini mtu mkweli
anaweza kusema kitu mara moja hata usipomuamini hatajali sana na ataendelea na
mambo yake.
Source: SIRI ZA AFYA BORA
0 Comments