Shirika la afya duniani linasema kwamba zaidi ya wanawake laki tano
waliuawa na kansa ya matiti mwaka 2011, idadi ya vifo hii hitegemewi
kupungua zaidi ya kuongezeka miaka inavyozidi kwenda mbele...
Kutokana
na hali hii njia mbalimbali zimekua zikitumika kujaribu kugundua kansa
hizi mapema na kuzitibu kabla hazijafika hali mbaya zaidi.
Unaweza kufika kwenye hospitali mbalimbali ukafanyiwa kipimo cha
kuangalia uvimbe kwa kupapasa kwa kutumia mikono ya daktari au vipimo
maalumu vya mionzi.
Kama wewe ni msichana au mwanamke basi ni vizuri ukaweka utarativu wa kwenda kupima kansa ya matiti anagalau kila baada ya miezi sita na kama huwez kwenda hospitali basi leo ntaenda kufundisha jinsi ya kujikagua ili ukigundua uwahi hospitali, kumbuka katika hatua za mwanzo kabisa za kansa mgonjwa anaweza kutibiwa na kupona kabisa lakini ikishasambaa mwili mzima inakua ngumu kidogo kumsaidia mgonjwa kama huyo..
zifuatazo ni hatua tano za kujikagua matiti yako
hatua ya kwanza;
ukiwa kifua wazi simama mbele ya kioo huku umeweka mikono kiunoni kisha angalia kama kuna vitu vifuatavyo
- angalia kama matiti yako yamebadilika rangi, shepu au ukubwa...kwa hali ya kawaida matiti hufanana kwa kila kitu bila uvimbe au chochote.
- ukiona mabadiliko ya ngozi kwa hali yeyote ile, chuchu kuvimba au kutumbukia ndani, wekundu au upele basi nenda hospitali upesi..
hatua ya pili..
inua mikono kwenda juu na uangalie tena, hapa angalia kama kuna majimaji
yeyote yanayotoka kwenye matiti...inaweza kua maziwa, maji au damu na
ukiona maji ya aina yeyote na rangi yeyote vinatoka nenda hospitali
haraka.
hatua ya tatu;
sasa lala kitandani na uanze kuyatomasa maziwa yako kwa kutumia mikono
na kwa ziwa la kushoto tumia mkono wa kulia na ziwa la kulia tumia mkono
wa kushoto..
hapa unaweza kutumia njia tatu kuu, kwanza unaweza kuanzia kwenye chuchu
na kutomasa kwa duara kwenda nyuma mpaka ufike mwisho wa titi, pili
unaweza kutomasa kama unapanda na kushuka mwinuko wa ziwa tatu unaweza
kutomasa kwanzia ndani kwenda nje moja kwa moja kama picha
zinavyoonyesha hapo...hakikisha unakandamiza vizuri mpaka ndani kabisa
ya ziwa na ukihisi vitu kama vya duara ndani ya ziw, ugumu kwenye ngozi
au kitu chochote ambacho mwanzoni hukua nacho wahi hospitali..
hatua ya nne;
simama na uyakague matiti kama jinsi nilivyoelekeza kwenye hatua ya
tatu, wanawake wengi hupendelea kufanya hivi wakiwa wameloa maji kwenye
matiti hasa kwenye hatua hii ya kusimama hivyo unaweza kufanya hivi
ukiwa bafuni tu.
mwisho; maelekezo niliyotoa hapo ni mepesi sana na muda mchache
sana unaweza kutumika kufanya kazi hii lakini ukipuuzia unaweza kupoteza
maisha, kumbuka unaweza kujipima angalau mara mbili au mara nne kwa
mwaka yaani kila baaada ya miezi mitatu mpaka sita na kila mwanamke yuko
hatarini kupata kansa ya matiti.
Kwa maelezo zaidi juu ya masuala ya Afya Bonyeza hapa >> SIRI ZA AFYA BORA
0 Comments