Inasemekana mahali hapo alifika Mzungu aliyeitwa James, hivyo huyu Mzungu akataka watu wamwiite "J" badala ya kutamka jina lote. Hivyo akawaambia CALL ME J, wabantu wakatamka KOLOMIJE na kutengeneza jina la eneo hilo.
2. KARIAKOO
Hii ilitokana na neno #Carrier_crop ambalo lilikuwa ni jina la wabeba mizigo wa eneo hilo la sokoni, lakini Waswahili walishindwa kulitamka jina hilo hivyo wakasababisha kutokea kwa jina la Kariakoo.
3. MSASANI.
Hili jina lililotokana na Bwana mmoja aliyeitwa Musa Hassan ambaye alikuwa ni Mnyapara aliyekuwa akisimamia mashamba ya katani ambaye asili yake ni Ntwala, wamakonde wengi wakaamua kuja kumuomba kazi na kwa kwa kuwa walikuwa hawajui anapoishi waliuliza kwa Mucha Hachani, na wakaendelea kuunga unga mpaka kusababisha kutokea kwa jina la Msasani.
4. KAWE.
Hili lilitokana na neno #Cow_Way, barabara maarufu kwa kusagwa ng'ombe kufikishwa hapo Tangaynyika Packers kwa machinjo.
5. KIGOGO
Ilitokana na kigogo halisi kabisa cha kuvuka pale kigogo mwisho kila jumamosi walikuwa wanakusanyika kukiweka "jamani leo siku ya kigogo" (leo pamejengwa daraja).
6. TABATA
Palikuwa na Muarabu aliyekuwa ananunua korosho kwa mali kauli na kuwaahidi wachuuzi waje siku fulani watalipwa kwa kuwaambi "hapana tabu tabata (utapata pesa yako) akabatizwa jina la Mwarabau Tabata, na mwishowe mahali hapo napo pakaanza kuitwa Tabata.
7. ILALA
Jina hili linatokana na makaburi ya pale Karume ambako hakukua na mengine hivyo kila alasiri watu walikuwa wakienda kuzika na wimbo wa Haila Illallah! na mwishowe mahala hapo pakaanza kuitwa Ilala.
8. UBUNGO
Majina yafuatayo: bungoni, mikoroshini, na mabibo yote haya yalitokana na uwepo wa miti mingi ya matunda hayo kupatikana maeneo hayo.
9. KIBORILONI
Kiboriloni ni neno lililotokana na maneno mawili KIBO na ALONE. Hii ilikuwa sehemu ambapo wazungu walisimama na kuona kilele cha Kibo pekee bila kukiona kilele cha Mawenzi, Kibo na Mawenzi ni vilele vya Mt. Kilimanjaro.
10. KIBOSHO
Lilitokana na maneno KIBO na SHOW, hii ni sehemu ambapo Kibo kilionekana vizuri zaidi.
11. MWANANYAMALA
Hapo kitambo mitaa ya MwanaNyamala kulikuwa na mapori na wakabaji, kwa hiyo kina mama wa kizaramo walivyokuwa wakifika mitaa hiyo wakawa wanawaambia watoto wao "Mwana Nyamala" maana yake "Mtoto Nyamaza" ili wasisikiwe na maharamia.
12. TABORA
Kambi ya Wafanyabiasha. Walikuwa wakipita na bidhaa zao wanakuta viazi vitamu vilivyopikwa na kukatwakatwa vipande na kuanikwa. Hapo huliwa makavu (Chewing gum) au kupikwa na kuliwa. Haya huitwa Matobolwa au Matovola. Hivyo wakapaita kambi ya Matobolwa au Matovolwa. Hii ilikuwa kugeuka na kuwa Tabora.
13. SUMBAWANGA
Wenyeji wa maeneo hayo walikerwa na vitendo vya ushirikina (tofauti na mtazamo wa watu wengi kwamba wenyeji wanaendekeza ushirikina). Kutokana na kero hiyo waliamua kuwapiga mkwara watu wanaoingia katika mji huo kwamba kama unataka kuja huku, basi Tupa Uchawi i.e Sumba (Tupa) Wanga (Uchawi), ukitupa na kuuacha uchawi wako huko uliko unaruhusiwa kuja hapo Sumbawanga.
14. MTONI KWA AZIZ ALI.
Mtoni kwa Aziz Ali pamepata jina kutokana na mkazi mmoja aliyekuwa maarufu (alwatani) sana marehemu Aziz Ali. Mzee huyu alifariki miaka kadhaa iliyopita.
15. KWA BIBI NYAU.
Kwa Bibi Nyau kulikuwa na ajuza mmoja alikuwa anafuga paka wengi sana.
16. NEWALA.
Waingereza walipofika Mtwara walikuta kisima kilichojengwa na wajerumani ambacho kilikuwa cha kizamani kwa wakati Huo , Hivyo walijenga kisima kipya na kukiita NEW WELL, watanganyika wakatamka NEWALA, hatimaye likawa jina la ile sehemu.
17. CHEKERENI[MOSHI].
Hili ni eneo ambapo barabara inakatiza kwenye reli.Sasa wazungu waliweka alama ya bararani ya tahadhari kabla ya kuvuka reli CHECK TRAIN, watu wakatamka CHEKERENI na kuliita hivyo lile eneo hadi leo.
#PIA UNAWEZA UKACOMMENT VYANZO VYA MAJINA MENGINE UNAYOYAFAHAMU.
Source: Habari Forums
0 Comments