Habari

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Advertise with us here

Bill Gates: Kosa kubwa la muda wote ni kuiacha Android kuongoza

Bill Gates

Katika mahojiano ya hivi karibuni, mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft, Bill Gates amenukuliwa akisema kuwa katika moja ya kosa lake kubwa la wakati wote alilolifanya ni kuiacha Android kuongoza katika mifumo ya uendeshaji Duniani.

Amesema katika ulimwengu wa programu anayeongoza katika kuwa na programu endeshaji inayotumika kwenye vifaa vingi zaidi ndiye anakuwa mshindi wa masoko yote. Hivyo kwa upande wa Microsoft imefanya kosa kubwa ambalo limeifanya Android kuongoza sokoni.
Android kwa sasa ndio mfumo endeshi unaoongoza kwa kutumiwa na watu wengi zaidi duniani ukifuatiwa na mfumo wa Microsoft, yaani Windows.

Microsoft ilijaribu kuleta programu endeshaji spesheli kwa ajili ya simu iliyokwenda kwa jina la Windows Mobile kwa upande wa simu zake za Windows Phone lakini haikupokelewa vizuri sokoni na pia kwa watengenezaji wa apps. Microsoft ikajikuta bado inabaki ikitamba katika kompyuta zaidi.
Kwa sasa Android inatumika katika 85% ya simu janja zote duniani.
Google walinunua kampuni ya iliyokuwa inatengeneza programu endeshaji ya Android mwaka 2005 kwa dola milioni 50 mwaka 2005 hii ikiwa ni miaka miwili nyuma kabla ya Apple kuja na iPhone mwaka 2007, na simu ya kwanza inayotumia Android iliingia sokoni mwaka mmoja baada ya iPhone – mwaka 2008.
Apple kupitia iOS na Google kupitia Android walibadilisha kabisa mtazamo wa biashara za simu, na apps – makampuni kama vile Microsoft, Nokia na BlackBerry walichelewa kubadilika na hii hivyo kujikuta nyuma kimaendeleo katika sekta hii.

Microsoft ishakata tamaa katika soko la programu endeshaji ya simu, tayari washatuma ujumbe kwa watumiaji wake wa simu za Windows 10 Mobile ya kwamba kufikia Disemba mwaka huu hawataweza kupata masasisho tena ya programu endeshaji yao na hivyo waamie kwenye simu za Android au iOS.

Chanzo: TEKNOKONA

Post a Comment

0 Comments

Youtube Channel Image
Hajiizo Subscribe To watch more
Subscribe