Kumegunduliwa powerbank ambazo zinaokoa
sana watumiaji wa smartphone, lakini ubunifu haujaishia hapo… sasahivi
zimekuja mpaka jeans, ndio…. Unavaa suruali yako fresh kabisa alafu
unatundika na smartphone yako na betri yake inaendelea kuingiza chaji
mdogomdogo!
Jeans yenyewe imeingizwa sokoni Marekani
kwa dola 189 (Tshs. 400,000/= kwa sasa), utaweza kuchaji smartphone
yako alafu kila kitu kinakuwa sawa… usihofu kwamba simu yako itaanguka,
kuna sehemu poa ya kuweka simu pamoja na betri yenye chaji ili iendelee
kuchaji simu yako popote ulipo.
Sehemu ya kuweka simu ni kama kimfuko
hivi juu ya mfuko wa nyuma wa jeans, ila kama simu yako ni kubwa kuliko
iPhone 6 basi itakuwa bahati mbaya yako, haitoweza kuingia.
Cheki video hapa ikionesha namna jeans hiyo ilivyotengenezwa >> VIDEO
Source: Millardayo
0 Comments