Mahakama ya juu zaidi nchini Uganda imesema kuwa utamaduni wa kurejesha
mahari baadaya talaka katika ndoa za kitamaduni unakiuka katiba na
utamaduni huo unapaswa kupigwa marufuku.
Uamuzi huo wa majaji saba katika mahakama hiyo umetolewa baada ya
wanaharakati wa haki za wanawake kuwasilisha kesi mahakamani wakisiema
kuwa utamaduni huo unawanyima wanawake haki zao.
Jaji mkuu wa
Uganda Bart Magunda Katureebe amesema kuwa ikiwa utamaduni huo
utaruhusiwa kuendelea itakuwa na maana kuwa wanawake ni kama bidhaa
zinazouzwa sokoni. Lakini idadi kubwa ya majaji hao
walikubaliana na uamuzi kwamba utamaduni wa utoaji mahari unapaswa
kuendelea na kwamba haukiuki katiba.
Hata hivyo mmoja wa majaji
hao alisema kuwa utamaduni huo unawadhalilisha wanawake na kwamba
mahakama inapaswa kulifanya swala la ulipaji mahari kuwa chaguo na wala
sio sharti.
0 Comments