Habari

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Advertise with us here

Uzinduzi wa Windows 10 ni mwanzo mpya

Programu ya Windows 10 imeadhimisha mwanzo mpya katika kompyuta za kibinafsi ,kulingana na mtendaji mkuu wa kampuni ya Microsoft .
Programu hiyo ilizinduliwa kimataifa siku za hivi karibuni, na ni jaribio la kampuni hiyo kujaribu bahati yake katika sekta ya simu.
Windows 10 itatolewa bure kwa wateja wengi kama hatua ya kuboresha programu hiyo.


Hata hivyo makampuni yatalazimka kulipia toleo hilo jipya hivyo watengenezaji wa PC watahitajika kuiweka katika vifaa hivyo.
Wachambuzi wanasema mkakati huo umezinduliwa ili kuharakisha utumizi wake.
Alipofanya mazungumzo ya kipekee na BBC, Satya Nadella alisema ''programu ya windows 10 ni hatua kubwa kwetu sisi kama kampuni, na katika sekta nzima''.
Microsoft imekua mbioni kuizindua kwa muda wa wiki kadhaa zilizopita, hivyo si kila mtu atapata fursa hiyo ya kuboreshewa siku ya kuanzishwa kwake

chanzo: bbcswahili.com

Post a Comment

0 Comments

Youtube Channel Image
Hajiizo Subscribe To watch more
Subscribe