Habari

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Advertise with us here

SIASA: Prof. Lipumba ajiuzulu uenyekiti CUF

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba leo ametangaza kujiuzulu uenyekiti ndani ya chama hicho.
Tamko hilo la Prof. Lipumba linahitimisha siku mbili za minong’ono na tetesi zilizogubika medani ya kisiasa nchini kuwa kiongozi huyo anaondoka katika chama hicho hali iliyolazimu wananchama, wapenzi na mashabiki wa kiongozi huyo kufurika makao makuu ya chama hicho Buguruni Dar es Salaam jana ili kujua hatma ya kiongozi wao huyo.
Akizungumzia sababu za kujiuzulu kwake, Profesa Lipumba amesema amekerwa na hatua ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao CUF ni chama shiriki kushindwa kusimamia makubaliano yaliyopelekea kuundwa kwa umoja huo.
Amesema Ukawa ulianzishwa kulinda maslahi ya wananchi yaliyoainishwa kwenye Katiba iliyowasilishwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba, na kwamba nafsi yake inamsuta hivi sasa kuendelea na uongozi huku waliokuwa wanaipinga Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba wakikaribishwa kuwania uongozi wa nchi kupitia umoja huo.
Prof. Lipumba amesema baada ya kujiuzulu atajikita kufanya shughuli za kitaaluma kwa kujihusisha zaidi na ushauri wa masuala ya uchumi na maendeleo.



Post a Comment

0 Comments

Youtube Channel Image
Hajiizo Subscribe To watch more
Subscribe