Habari

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Advertise with us here

Samsung wamekuletea Technology ya kuzuia ajali barabarani kupitia malori

Kupitia kitengo chao cha utafiti wa kiteknolojia kampuni ya Samsung imekuja na teknolojia inayoweza kusaidia kwa kiasi kikubwa utokeaji wa ajali zinazohusisha watu kutaka kuyapita malori (ku-overtake). Ajali nyingi katika nchi zinazoendelea huwa zinatokea katika ku-overtake malori malefu bila kuona vizuri kinachokuja kwa mbele.
Teknolojia hii inahusisha utumiaji wa kamera spesheli zilizopo mbele ya roli na kuonesha kupitia TV kubwa inayokuwa sehemu ya nyuma ya lori. Wamedai TV hiyo iliyotengenezwa spesheli ina vioo spesheli za kuifanya iwe salama dhidi ya uvunjikaji wa kirahisi, pia kamera hizo zitaweza kuonesha vizuri ata wakati wa usiku.
Waandishi wengi wametoa sifa kwa kampuni hiyo kwa wazo hili la kitofauti.
Samsung wanasema teknolojia hii itaweza kusaidia ajali za aina mbalimbali, kama vile kujua gari linalokuja kabla ya kufanya maamuzi ya ku-overtake.. pia ajali zinazotokana na malori kufunga breki za ghafla kutokana na wanyama au watu kuvuka barabara ghafla. Kamera na tv zake za nyuma zinaweza kufanya kazi ata usiku.
Kwa sasa Samsung wamefanikiwa kufanya majaribio ya teknolojia hiyo nchini Argentina ambayo ni moja ya nchi zinazoongoza kwa ajali za malori na hadi sasa wengi wameisifia sana teknolojia
hiyo. Kilichobaki kwa sasa majaribio zaidi na wao kufanya maboresho na kisha kuomba kibali rasmi katika nchi mbalimbali ilikuweza kupata baraka ya utumiaji wa teknolojia hiyo.
Gari hizi zimepewa jina la Samsum safety truck. Tupe maoni yako kwa hili

Post a Comment

0 Comments

Youtube Channel Image
Hajiizo Subscribe To watch more
Subscribe