Watumiaji wa Android na wa huduma za WhatsApp na Viber wamerahisishiwa zaidi kutuma ujumbe wa pupa, kama wanajua kutumia kipengele cha ‘OK Google’ kwenye Google Now.
Kipengele hichi cha OK Google kinatumika
kuamuru simu ya Android na hata kivijari cha Google Chrome kufanya mambo kadha
wa kadha. Kwenye simu yako kwa mfano, unaweza kuitumia kutafuta vitu kwenye
Google, kuweka alamu, kuandika SMS na barua-pepe, kupiga simu na kadhalika.
Mapema mwaka huu, Google ilitangaza kwamba
itaruhusu app zingine kutumia uwezo wa Google Now kurahisisha matumizi ya
Simu yako. Sasa, Google Now inaweza kutumika kutuma ujumbe sio tu kwa WhatsApp
na Viber, bali hata kwa WeChat, EndeleaPlus na Telegram pia. Unachotakiwa
kufanya ni kusema kitu kama ‘OK Google’, ‘Send WhatsApp message to Eric,’ alafu
utaulizwa ujumbe unaotaka kutuma. Sema ujumbe wako na ujumbe wako utakuwa
umetumwa. Unaweza kuangalia video hapo chini.
Hata hivyo, kuanza kutumia WhatsApp kwenye simu yako, yakupasa kusasisha
WhatsApp pamoja na app ya Google na kuiwezesha simu yako kutumia ‘OK Google’
kwenye mipangilio ya app ya Google. Ilani: Lugha ambayo inatumika kwa sasa ni
kiingereza na lugha nyingine chache zilizokomaa kwenye kipengele cha ‘OK
Google’.
0 Comments