Facebook imeamua kumruhusu kila mtu aamue ni habari za aina ipi anataka kuziona kwenye kurasa yake. Hii inawezekana kwa kipengengele kipya walichokiongeza, kinachokuruhusu kuchagua marafiki wako unaopenda kuona habari zao awali ya habari zote zingine kwenye kurasa yako punde unapoingia kwenye mtandao huo wa kijamii.
kuu ya badiliko hili jipya kutoka Facebook ni kwamba
huna haja ya kushuka chini sana kwenye skrini ama kurasa yako kuona habari
unazopenda zaidi. Hili ni jambo la kitofauti sana kutoka kwa Facebook, kampuni
iliyozoeleka kuwa na usiri wa hali ya juu kuhusu namna wanavyochagua
kukupa habari za marafiki na kampuni upendazo na wanafanya hivi kupitia kitu
kinachojulikana kama ‘The Facebook Algorithm’ . Ili kutumia mabadiliko ya
Facebook yaliyoelezwa hapa, ingia kwenye News ‘Feed Preferences’, chaguzo iliyo
ndani ya menu karibu na eneo la taarifa pale juu, kulia kwenye kurasa au app
yako ya facebook.
Utaona orodha ya watu ama kurasa uloziziona karibuni
au zile unazozitembelea mara nyingi.
Ukifanikiwa kuchagua mipangilio ya kukufaa,
utaweza kuona habari za hao marafiki na kurasa uzipendazo kwanza kabla ya
habari za watu wengine. Kwa kweli, kwa hili la kitofauti la kutoka kwa
facebook, unaweza kuona kidogo faida au labda tuseme raha, ya Facebook kwani
utapata muda wote kile unachotaka.
Kwa ujumla hii ni habari nzuri, na pengine cha
kufurahisha zaidi ni kwamba chaguo lako la watu unaotaka kuona ni siri yako,
halitojulikana kwa wengine. Hakuta kuwa na wasiwasi kwamba mtu mwingine atajua
kwamba hauwekei maanani ‘update’ zinazotoka kwake.
2 Comments
Ahsante kwa kushare na cc...
ReplyDeleteyou are almost welcome
Delete