Habari

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Advertise with us here

Zaidi ya wahamiaji 200 waangamia Libya

Zaidi ya watu mia mbili wanahofiwa kufariki baada
ya boti mbili iliyokuwa imebeba wahamiaji haramu
kuzama katika eneo la Zurawa pwani ya Libya.
Mamia ya wahamiaji wengine wameokolewa na
wanamaji wa Libya usiku wa kuamkia leo.
Kwa zaidi ya mwaka mmoja Libya haijakuwa na
serikali dhabiti na sehemu kubwa ya nchi hiyo
inathibitiwa na wanamgambo wa Kiislamu, na
walanguzi wa watu wanatumia fursa hiyo
kusafirisha watu kimagendo hadi Ulaya.
Kwa mara ya kwanza wakaazi wa mji huo
waliandamana kupinga usafirishaji wa watu kupitia
mji huo.
Ripoti zinasema kuwa meli mbili zilizokuwa
zimebeba wahamiaji hao zilizama muda mfupi tu
baada ya kunoa nanga.
Meli moja inasemekana kuzana usiku wa kuamia
siku ya Alhamisi na nyingine saa chache baada ya
tukio hilo.
Kwa mujibu wa afisa mkuu wa shirika la uhamiaji la
kimataifa IOM, nchini Libya, watu mia moja tayari
wameokolewa na kusafirisha hadi kambi moja ya
muda iliyoko mji wa Sabratha.
Amesema wengi wa manusura hao ni wanaume
lakini wamefanikiwa kuwaokoa wanawake tisa na
watoto wawili.
Vyanzo vya habari mjini Zuwara zinasema kuwa
miili ya watu mia moja zimehifadhiwa katika
hospitali moja mjini humo.
Walioangamia kwenye ajali hiyo ni raia wa Syria,
Bangladesh na mataifa kadhaa ya Afrika.

Nini maoni yako kuhusu hili?

source: bbcswahili.com

Post a Comment

0 Comments

Youtube Channel Image
Hajiizo Subscribe To watch more
Subscribe