ni ndoto ya kila binadamu kuishi maisha marefu na yenye afya, kimsingi
hakuna binadamu angependa kuishi maisha mafupi na yenye afya mbovu
lakini kulingana na asili ya dunia yetu kuna changamoto nyingi sana za
magonjwa na ajali ambazo zimepunguza urefu wa maisha wa binadamu
wengi.vipo vyanzo vya vichache vifo ambavyo kimsingi haviepukiki lakini
vyanzo vingi vinaweza kuepukika na kuongeza urefu wa maisha yako hapa
duniani. yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia ili kuishi maisha
marefu.
acha ulevi; unywaji wa pombe kupita kiasi una madhara makubwa kwa
binadamu. madhara ya kifedha yaani kufilisika na na madhara ya kiafya.
pombe ina haribu maini kwa kiasi kikubwa sana na baadae heleta kansa ya
ini ambayo imeua vijana wengi wadogo.kama unapenda pombe basi kunywa
kiasi kidogo na nyakati maalumu na haitakudhuru. lakini pia wasichana
wengi wamejikuta wakifanya ngono mpaka na watu ambao hawakuwategemea
sababu ya ulevi.
acha ngono zembe; tabia ya kufanya ngono na wanawake tofauti bila
kinga haitakufikisha mbali, ukimwi umeua vijana wengi sana na sio
rahisi kujua kwani hua ni siri ya familia siku ya mazishi na kama huwezi
kutumia kondom basi tafuta mpenzi mmoja muaminifu na utulie
naye.utafiti unaonyesha wanawake wmeathirika sana na ukimwi, pamoja na
sababu zingine za kitaalamu lakini hofu yao ya mimba ni kubwa sana
kuliko ukimwi.
kula vizuri; hakikisha kabla hujala chakula chochote unatafakari
kama kina faida yeyote kwenye mwili wako, ulaji wa vyakula ambavyo
havina faida mwilini kama pipi, biscuit, soda, na jamii zake vitakuua na
kansa siku za usoni lakini pia unene ambao kimsingi huletwa na kula
sana utakuletea magonjwa hatari kama kisukari na magonjwa mengine ya
moyo.
tumia vyombo vya moto kwa uangalifu; matumizi ya vitu kama gari
na pikipiki yanahitaji umakini mkubwa sana hasa ukiwepo barabarani,
vijana wengi wadogo wameuawa na vyombo hivi.epuka kuendesha gari
umelewa, epuka mwendo mkali, vaa helmet wakati wa kuendesha pikipiki,
vunga mkanda wewe dereva au abiria na usikubali kubebwa kwenye gari au
pikipiki na mtu ambaye hathamini maisha yake.usione aibu kumwambia
dereva apunguze mwendo kwani umemlipa na ameshika maisha yako. na wewe
usiyejua kuvitumia kajifunze kwanza chuoni ndio uanze kuvitumia.
shiriki mazoezi; magonjwa ambayo sio ya kuambukizwa kama
kisukari, ugonjwa wa moyo, na presha husababishwa sana na maisha ya
uvivu. binadamu anatakiwa afanye mazoezi angalau nusu saa kwa siku.
visingizio kwamba uko bize sana ni dalili ya kukosa vipaumbele na
nidhamu kwenye maisha yako.hizo hela unazotafuta usiku na mchana
usipokua na afya bora utakufa uziache.
epuka ugomvi usio na maana; mimi nafahamu watu waliopigwa ngumi
moja tu wakafa hapohapo. mwili wa binadamu ni mlaini sana. kuna sehemu
ambazo zikipigwa unakufa hapohapo. jitahidi kua mtu wa kusuluhisha zaidi
kuliko kukunja ngumi.watu wote waliouawa kwa kuchoma visu au kupigwa
mawe walikufa kwenye mazingira haya.kama umejifunza kupigana basi pigana
pale unapokua umeshambuliwa ili kujilinda sio kuanzisha ugomvi
makusudi.
usivute sigara; sigara ni moja ya starehe ambayo haina faida
yeyote kwenye mwili wa binadamu, huharibu seli za kwenye mapafu na
baadae huleta kansa ya mapafu.unaeza ukasema mbona fulani kavuta mapak
leo hajafa. kila mtu ana kinga yake ya mwili amabyo ni tofauti na
mwingine lakini pia hakuna anayechoka kuishi...huyo unayemuona anatamba,
siku akiambiwa sigara ndio iko inamuua hata kama ana miaka 90
atasikitika sana.
usijihusishe na madawa ya kulevya; madawa ya kulevya hayatakuua
hapohapo lakini yatakuondoa kwenye mkondo wa maisha ya mafanikio.
utadharaulika na kila mtu, utakua huwezi kufanya kazi, muda mwingi
utawaza kuiba ili upate madawa mengine ya kutumia.rafiki yangu mmoja
mwaka 2004 alivuta bangi kwa kama miezi sita tu akawa kichaa na hajapona
mpaka leo pamoja na kupelekwa hospitali nyingi za vichaa.unaweza ukaona
jinsi amegeuka mzigo kwa ndugu zake.
jiupushe na uvunjaji wa sheria za nchi makusudi; tabia za wizi,
dili za kihalifu, uuzaji wa magendo au kumuibia muajiri wako ii
ufanikiwe haraka hua hazina muda mrefu sana maishani. yaani huwezi ukawa
mjanja maisha yako yote kwani ipo siku utakamatwa tu.lepo hii kijana au
mtu mzima ukihukumiwa miaka 30 basi maisha yako yameishia hapo na
huenda ukafia gerezani. matajiri wote duniani wlianza miaka mingi
iliyopita. jifunze kua mvumilivu.
waheshimu wazazi wako; 'waheshimu baba yako na mama yako siku zako zipate kua
nyingi sio kuwaheshimu kwa
kuwapa shikamoo kila asubuhi bali kwa kufuata maelekezo na ushauri wao
kwani wao wameishi miaka mingi sana duniani na wameona mengi.
SOURCE: SIRI ZA AFYA BORA
1 Comments
nimeipenda hii..
ReplyDelete